Fahamu maana ya mithali 16:1″Nini maana ya ‘Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu’ ?”

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu kupitia jina la Mwokozi lenye nguvu, karibu tena katika kujifunza Neno la Mungu ..

Turejee

Mithali 16:1
[1]Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;
Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

Hapa aliposema maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, ni kwamba Mungu amempa kila mwanadamu mamlaka au nguvu ya kupanga mipango yake mwenyewe vile anavyotaka iwe katika malengo yake au maono

Mfano mtu anapanga, nikiwa mkubwa nitakapohitimu masomo yangu nitakuwa mwalimu, lakini badae inakuja kuwa ndivyo sivyo, kama ulivyopanga, anapata kazi ambayo hakuwahi hata kuifikiria, hii ndiyo maana ya maandilo ya mwanadamu

Lakini unapoona yale uliyoyapanga yamekuja tofauti na mipango yako, hilo ndilo jawabu la Bwana, kwa sababu ni kweli malengo yako ulivyopanga ni mazuri tena yana faida kubwa maishani mwako, lakini ukiona Mungu amelipindua basi jua hapo anakuwa ameandaa jambo zuri kuliko hilo, yamkini kama ungepata unacho kitaka ungemuacha Mungu au ungepata mateso.

Unapoona mambo haya yamekupata mipango yako haijatimia isiwe wakati wa kumlaumu/kumnung’umikia Mungu bali jua kabisa Mungu anakuwazia mema na jawabu linatoka kwake lililo bora

Ukilijua hili basi unapokuwa una panga mipango yako, panga lakini mwachie Mungu afanye kwa mapezi yake afanye  apendavyo yeye, usijiwekee asilimia zote kuwa kile ulichopanga itakuwa. Na malizia kwa kumwambia Bwana kwa imani kabisa na moyo mweupe kuwa “IKIKUPENDEZA BWANA MAPENZI YAKO YATIMIE KATIKA HILI/KATIKA HAYA NINAYOYAHITAJI”.

Hivyo tunapopanga mipango yetu yote tusijisahau kabisa na kujiwekea matumaini na uhakika katika hayo kwamba haliwezi likatanguka jambo lolote.  La! Maana kama tukienda na fahamu kama hizo tumaini letu litatoka kwa Bwana pale mipango yetu inaposhindwa kutimia.  Ikiwa Bwana yeye ajuaye mwanzo hata mwisho ikiwa ni mipango ambayo haitaadhiri maisha yako ya kiroho au mahusiano yako na yeye ataruhusu kabisa jambo hilo lifanikiwe lakini kinyume na hapo halitafanikiwa.

Si kwamba hapendi ufanikiwe katika hicho bali atakupa kilichobora zaidi.

Yakobo 4:13 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;

14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.

15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.

16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya”.

 

Hivyo kama watu tuliomwamini Yesu Kristo ni vizuri tukawa na maono na kuyaombea lakini mwisho wa yote tumuachie Mungu ajuaye yote na ANAETUWAZIA MEMA DAIMA.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *