Mwanadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa ni yupi?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu mpendwa tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana wetu yesu kristo.

Je? Wanadamu wa kwanza aliowaumba Mungu walikuwa wana namna gani? Walikuwa wa rangi gani?

Ni vyema tufahamu maandiko hayajaeleza shemeu yoyote kuwa mtu wa kwanza alikuwa mzungu,mwafrika,Mwarabu nk lakini aliumba watu wawili pale Edeni ambao ni Adamu na Hawa nao walikuwa ni jamii moja yaani Rangi ilikuwa moja tu. Wala Adamu na Hawa walikuwa na rangi moja.

Kama neno linavyosema

Mwanzo 1: 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba ).

Hawa wawili waliumbwa na Mungu kwa ukamilifu pasipo kasoro zozote Adamu na mke wake hawakuwa wazungu hapo mwanzo Adamu na Hawa walikuwa ni watu wenye upekee kulingana na uumbaji ambao Mungu aliufanya(Waliumbiwa miili ya tofauti kabisa ambayo hapo kwanza ilikuwa haina magonjwa na waliumbwq wala hawakuwa na asili ya dhambi yoyote  ndani yako kama ilivyo hivi leo.).

kwa hawa wawili kwakuwa walikuwa wenye muonekano mzuri mno pia walikuwa na mvuto sana kwakuwa Mungu aliwaumba katika ukamilifu. lakini baada ya Adamu na Hawa kumuasi Mungu na ule utukufu alioweka Bwana juu yao uliondoka na ndipo ulipokuwa mwanzo wa kuwa kama sisi.

Hii jamii ilianza kubadilika baada ya Mungu kuuondoa utukufu wake juu Yao ikapelekea ardhi kulaaniwa, jua kuwa Kali, mimea ikakauka na kuleta jangwa, walibadilika rangi na kupelekea baada ya gharika Dunia ilianza kubadilishwa mifumo na wanadamu wafumbuzi na hii ikapelekea watu kuishi maisha yanayomchukiza  Bwana.neno la Bwana linasema.

Mwanzo 11:1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.

2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.

3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.

4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.

5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.

6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.

7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.

8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.

9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.

Kuanzia hapo watu watu walitawanyika na walienda maeneo mbali mbali yaliyokuwa juu ua uso wa nchi kama vile maeneo yenye majangwa, misitu, porini,Joto,Baridi n.k walipoendelea kuishi huko kwa muda mrefu wakaanza kuendana na Yale mazingira ndipo ikaonekana tofauti ya watu kulingana na maeneo waliyoishi kwa muda mrefu.

Hivyo kwa ujumla mazingira ndiyo yanayowabadilisha watu na kugeuza miili  yao na kuishi kama wanavyoishi watumwa jamii husika.(Hivyo miili yao ilianza kuishi/kuendana na mazingira waliyokuwa wanaishi.. kama ilivyo kwa mwili wa mwanadamu huwa unaishi kutokana na mazingira fulani)

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *