Jina la Mwokozi wetu libarikiwe, karibu tena katika kujifunza Neno la Mungu..
Jibu; Hapana hakuna tofauti yeyote katika maneno haya mawili, lakini yana maana moja, na tafsiri ya jina hili ni “paradiso ya raha” hivyo maneno haya hayana tofauti yeyote
Ukisoma baadhi ya vifungu katika biblia utakutana na maneno haya mawili, Edeni na Adeni
Tusome
Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa EDENI, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya”.
Isaya 51:3 “Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama BUSTANI YA EDENI, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba”.
Katika vifungu hivi viwili vinaonyesha kuwa bustani aliyoiumba Mungu ilikuwa na jina la Edeni, lakini katika vifungu hivi vinaonyesha Adeni
Ezekieli 28:13 “Ulikuwa ndani ya ADENI, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari”
Yoeli 2:3 “Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na BUSTANI YA ADENI mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao”.
Hivyo basi, hakuna tafsiri tofauti katika maneno haya tofauti yake iko katika matamshi na herufi lakini yote yanamaana moja tu ambayo ni.. “Paradiso ya raha”
Ni sehemu ya kwanza kabisa kuwekwa mwanadamu kuwekwa baada tu ya kuumbwa na Mungu..
Na Mungu aliifanya/kutengeneza/kubuni hii bustani kwa wazazi wetu wa kwanza na alikusudia wawe na raha ya milele lakini baada ya kuasi, kwa kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya(waliasi/kukaidi amri au agizo walilopewa na Mungu) na kitendo hicho kikapelekea wao kufukuzwa au kuondosjwa katika makao hayo(Edeni/Adeni). Mungu alikusudia wawe pale milele lakini walivyokaidi utukufu wote ambao walikuwa wamepewa pale Edeni uliondoka.
Lakini kama tunavyojua Edeni yetu na Adeni yetu Bwana Yesu alienda kutuandalia baada ya kufufuka na kupaa mbinguni alikwenda kuandaa makao yetu na ndio maana anasema…”….nakwenda kuwaandalia makao (Yohana 14:2). ambayo ndiyo mbingu mpya na nchi mpya, na hii itakuwa ni kwa wale waliomokea Yesu Kristo maishani mwao; na kuoshwa kwa damu ya mwokozi wetu Yesu Kristo.
Je unatamani na wewe uwepo katika mbinguni mpya na nchi mpya na uishi maisha ya umiele yasiyokuwa na mwisho? Wala magonjwa wala ugomvi nk..?
Je nawe umemwamini Yesu Kristo ili siku ulimwengu huu utakapo haribiwa ukaione Edeni/Adeni, basi ikiwa Bado wakati ni sasa mwamini Yesu Leo ili uwe salama, na siku itakapofika uingie katika Mbingu mpya na nchi mpya
Maran atha
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.