Tusome
Kutoka 20:4“Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia”.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WANICHUKIAO,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Katika sura hii tunaona Mungu akitoa tamko juu ya watu wanaotenda nje ya agizo lake, ni nini atafanya , anasema “NAWAPATILIZA MAOVU YA BABA ZAO”
Maana halisi ya Neno kupatiliza ni kupiga au kuadhibu, sasa kutokana kifungu hicho hapo juu Mungu , alikuwa anamaanisha kuwa ikiwa na wazazi walikuwa wanatenda uovu kisha na watoto nao wakafanya hivyo, ndipo hapo akasema wanapatiliza wana..
Ndiyo maana hata tukisoma Habari wa wana Waisraeli, tunaona ilipelekea wanapelekwa utumwani ashuru na babeli, hii ilisababishwa na waflme wao, jinsi walivyokuwa wanafanya makosa mbele za Mungu kwa kuabudu miungu mingine na masamu, sasa hii ndiyo ilisabibisha tifa la Israeli kwenda utumwani
Lakini pia mpango wa Mungu si huu, wa kupatiliza uovu juu ya watu wake ndiyo maana ukisoma
Kutoka 20:6
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kumbe basi ikiwa ni kweli walifanya makosa,lakini kama ikitokea watoto wao wakafanya yale yanayompendeza mungu, Mungu hawezi kuwaadhibu bali anasemaa atawarehemu wampendao Bwana .
Hata kwetu pia ikiwa unaisha maisha sawa na wazazi wako walivyokuwa wanaishi maisha ya kutends dhambi, lazima atakipatiliza kizazi, lakini katika yote tunaposwa ikiwa tayari tumesha ijua kweli na tunaenda katikati mapenzi Bwana atarehemu
Ishi maisha ya kumpenda Mungu…
Ubarikiwe
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.