Bwana Yesu asifiwe
Katika Kifungu hiki baadhi ya mafundisho au tafsri mbalimbali za watumishi hualalisha unywaji wa pombe kuwa ni sawa tu kulingana na hiki kifungu, Je jambo hili lina ukweli ndani yake tusome
1Wakorintho 11:21 “kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu AMELEWA.
22 Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.”)
Sasa hapo aliposema kunywea hakumaanisha watu wanywe pombe, la si kweli, zaidi kitu alichokiwa anakizungumzia hapa paulo ni kuhusu HESHIMA YA NYUMBA YA MUNGU , mahali ambapo tunakusanyika kwa ajili ya ibada
Ndiyo maana hata mtume paulo, alitumia lugha ya ukali kuonyesha kuwa mambo haya kiuhalisi si mazuri mbele za Mungu wetu, mfano unakuta viongozi wa dini wanapingana ndani ya kanisani au wengine wanasengenyana, kwa vitu ambavyo havina msingi, sasa ni heri mambo yangefanyika nje ya nyumba ya Mungu, lakini unakuta ndani ya kanisani mambo haya yana fanyika ni jambo baya sana
Wakati mwingine watu wanageuza nyumba ya Mungu kuwa sehemu ya mitindo ya nguo, nywele, nk.. unakuta mtu haendi kanisani kwa ajili ya kumwabudu Mungu lakini anaenda kwa ajili ya ( fashion show)…
Kwa sababu mambo haya yalipaswa yafanyike sehemu nyingine na si katika nyumba ya Mungu, maana nyumba ya Mungu ipo maalumu kwa ajili ya ibada tu
Yohana 2:15-16
[15]Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;
[16]akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
Nyumbani mwa Bwana pana paswa paheshimiwe, ewe Binti, kijana usiende kanisani kwa sababu unataka mme au mke hiyo si sehemu ya kutafutia wake au waume bali ni maalumu kwa ajili ya ibada, hayo MENGINE huwa yanafuata baada ya kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza
Nenda nyumbani mwa Bwana kusudi lako likiwa katika kumwambudu Mungu na si mambo mengine, mashemasi, wazee wa kanisa, makatibu , wachungaji nk.. nyumba ya Mungu iheshimiwe ukitaka magomvi nenda nyumbani kwako ila si katika nyumba ya Mungu
Bwana atusaidie
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.