Shalom nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Jambo ambalo ni la muhimu na la kuzingatia, ni vizuri kufahamu biblia ilitafsiriwa kwa lugha zipi, au chimbuko gani la lugha ilitumika katika kuandika maandiko matakatifu ya Mungu,
Kipindi biblia inaandikwa haswa katika biblia yetu hii hususani agano jipya maneno mengi yaliandikwa kutoka katika lugha ya kigiriki, maana kwa ukubwa ilandikwa kwa lugha hiyo ya kigiriki, maana mfano lugha kama hizi hazikuchukua nafasi sana katika kuandika biblia mfano kifarasa, kichina, kilatini nk..
Je maana ya maneno haya Kristo na Kristu yana tafsiri tofauti..
Neno Kristo limetokana na neno la kigiriki yaani (Khristos) ambalo kwa biblia yetu ya kiswahili limaanisha KRISTO
Lakini Kristu limetoka na lugha kilatini (Christus) ambalo kwa lugha yetu ni KRISTU..
Lakini maana halisi ya Neno KRISTO NI MTIWA MAFUTA yaani MASIHI
Yohana 4:25
[25]Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
Hivyo haya maneno si kwamba yana maana tofauti maana yake ni ile ile tu, lakini kama nilivyo tangua kusema hapo mwanzo, tunapaswa kuzingatia lugha sahihi iliyotumia kuandika maneno ya Mungu, lugha ya kigiriki ndiyo ilichokuwa nafasi kubwa katika kuandika neno la Mungu, tuzingatie pia katika kuangalia lugha gani ilitumika…
Ubarikiwe
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.