Andiko hili limekuwa likitafsiriwa tofauti na lilivyo, lakini Leo tutajifunza linamaanisha nini/maana yake ni nini?
Mithali 24:26 “Aibusu midomo atoaye jawabu la haki”
Jawabu la haki linalomaaniashwa hapa ni kuwa mtu yeyote mwenye haki, ni yule anayeamua Kufunguka kwa wenzake kwa kumweleza ukweli wote pasipo kumficha jambo lolote ili kumweka huru na kumuepusha na jambo fulani baya, sasa huyu anatafsirika kama mtu mwenye upendo aliye toa jawabu la haki
Lakini ili kuelewa zaidi kuhusu haya maelekezo ya jawabu la haki tufahamu nini maana ya “aibusuye midomo”,
Tofauti na inavyodhaniwa katika neno hili siyo kule kunakomaanishwa kubusu katika nyakati hizi, maana hudhahaniwa kuwa jambo hili hufanyika pale watu wanapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi, lakini si hivyo
Ukweli ni kwamba, katika tamaduni za wahuyudi hii ilikuwa desturi yao ya kumbusu mtu, na hii ilikuwa ishara ya upendo wa dhati kwa huyo mtu, ndiyo maana walikuwa wanafanya hivyo
Ndiyo maana ukisoma baadhi ya maandiko katika biblia, utaona mitume walikuwa wanatoa agizo watakatifu wafanye hivyo
1 Wakorintho 16:20-21
[20]Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.
[21]Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe.
Tusome tena
2 Wakorintho 13:11-13
[11]Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
[12]Salimianeni kwa busu takatifu.
[13]Watakatifu wote wawasalimu.
Lakini sisi busu letu Leo ni kushikana mikono na kukumbatiana huku nako ni kuonyesha upendo wa dhati kwa ndugu zetu..
Tukirudi katika maana nzima ya mstari huo, aibusuye midomo hutoa jawabu la haki, haki yetu nasi tunaionyesha kwa kuwapenda watu kwa dhati kwa kuwaambia ukweli ili waponyeke, usiishie kusema tu kwa mdomo kuwa nampenda kwa dhati bali toa jawabu la haki kwa kuonyesha upendo wa kweli, usifurahi kuona ndugu yako anapotea alafu Unasema unampenda, hapo hakuna ukweli wowote
Bwana akubariki, tuzidi kuelewa neno lake
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.