Yesu ni Mungu au nabii?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mwana wa Mungu karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa mwokozi wetu Yesu Kristo.

Neno la Mungu linaonyesha kuwa Mungu ni nabii ikimaanisha kuwa ni kiongozi anayesimamia na kuliendesha kundi kubwa la watu wenye misimamo na mitazamo tofauti kulingana na lugha, tabia na mwenendo.hata kwa Mungu wetu itoshe kusema kuwa yeye ni nabii kwakuwa analiongoza kundi kubwa la watu.

Hivyo kristo akiwa hapa duniani anaitwa mwokozi na nabii pia Hali ya kuwa akiwa ndani yetu yeye ni Roho Mtakatifu neno la Bwana linasema.

Luka 24:19 “Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, ALIYEKUWA MTU NABII, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote”

Kumbukumbu 18:15

Kumbukumbu 18:15 “Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye”.

Pia maandiko yanasema Yesu ni mwana wa Mungu kama neno linavyosemwa.

Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni

Hivyo inatupasa tujue kuwa Yesu ni mwokozi wetu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *