Je mvinje ni mti gani?

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Mwokozi wetu Yesu lisifiwe, Karibu the jifunze neno lake lililobeba uzima ndani yake…

Swali: Je huu mti wa mvinje ulikuwa ni mti gani?

Jibu: Kulingana na maandiko mti huu tunausoma katika habari ya Nuhu baada ya Mungu kumpa maagizo atengeneze safina kwa kutumia mti huu wa mvinje

Mwanzo 6:13-14

[13]Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.

[14]Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.

Kwanini Mungu alimpa maelekezo wakati wa kujenga safina atumie mti huu na si mti mwingine, tutazama sifa ya mti ya mti huu….

Kwanza kabisa mti huu unapatikana sehemu kubwa ya duniani, ikiwemo bara la afrika, Mti huu una sifa ya kipekee maana una uwezo wa kuvumilia maji kwa mda mrefu bila kuharibika au kuonza kama miti mwingine, na pia ni mgumu sana..

Na mara nyingi mti huu hutumika kutengeneza barabara ya treni, au zile boti ambazo wavuvi hutumia kuvulia samaki, kwa sababu uwezo wake wa kuhimili maji kwa kipindi kirefu bila kuharibika..

Ndiyo maana Mungu alitaka Nuhu atumie mti huu, maana mvua ilinyesha kwa siku siku 40, na maji hayo yalidumu katika uso wa nchi zaidi ya siku 150, hivyo kama mti huu ungekuwa mlaini usingeweza kustahimili mbao zake zingeharibuka tu…

Mti huu unafunua jambo gani katika Roho zetu

Mti huu wa mvinje unawakilisha msalaba ambao ulibeba dhambi zetu, ukatusafisha makosa yetu hata Leo tupo huru, na safina yetu ni Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikubali kusulubishwa juu ya mti huo ili sisi wanadamu tuokolewe …NI NEEMA AJABU TUMEPENDWA UPEO

 

Wakolosai 2:14

[14]akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

JE umemwaminj Yesu Kristo maishani mwako, mwamini Leo ili uwe salama..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *