Nakusalimu kupitia Jina la Yesu, ndugu Karibu katika kipindi kingine ili tuweze kutafakari maneno ya uzima…
SWALI: Je kutokana ni kile alichokifanya sulemani, kufanya kosa la kuwajengea miungu madhabahu, baada ya kushawishiwa na wake zake,.sasa kupitia jambo hili sulemani hakusamahewa kabisa hiyo dhambi
1 Wafalme 11:4-9
[4]Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
[5]Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.
[6]Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
[7]Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.
[8]Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.
[9]Basi BWANA akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha BWANA, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,
JIBU: Ndiyo sulemani alienda Mbinguni, tunalithibitisha hili katika kitabu cha mhubiri
Tusome
Mhubiri 1:1-3,8-9
[1]Maneno ya Mhubiri, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu
[2]Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.
[3]Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
[8]Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
[9]Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.
Hapa ni baada ya sulemani kuyachunguza yote na kugundua kuwa, chini ya jua mambo yote ni ubatili hakuna lililo njema, alimalizia kwa kusema jumla ya mambo yote hapa duniani ni kumcha tu Bwana, hivyo sulemani baada ya kutambua makosa yake alitubu, ndiyo maana hata katika kitabu cha ukoo wa Yesu ametajwa pia
Mathayo 1:6
[6]Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;
Lakini jambo ambalo tunapaswa kujifunza katika habari ya sulemani, siku zote za maisha yetu, utii na jambo la muhimu, japo kweli sulemani alikuwa na hekima lakini alidondoka katika dhambi na hii ilisababishwa na kukosa utii wa maagizo ya Mungu, vivyo nasi tusijisifie utumishi wetu au maarifa yetu, na kutenda mambo yasifaa mbele za Mungu zaidi tunahitaji unyenyekevu na utiifu kwa Mungu wetu , taama zote za ulimwengu huu ni ubatili tu lakini katika jumla ya mambo yote ni kumcha Mungu ( mhubiri 12:13)
Bwana Yesu atusaidie
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.