Yesu Kristo, kwanini aitwe mwana kondoo?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe, karibu tujifunze neno la Mungu

Yesu Kristo alijulikana kwa sifa nyingi sana, mfano anajulikana kama simba wa yuda, maji ya uzima, mwamba imara nk… Hizi ndiyo tabia ambazo zilimtambulisha Yesu Kristo

Likini Leo tutajifunza sifa yake moja, Yesu Kristo kwanini aitwe mwana-kondoo na si mwana- mbuzi au mwana mbuzi au mwana- beberu.

Tusome

Yohana 1:29 “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”.

 

Kwanza kabisa tutazame sifa ya kondoo

  1.  kondoo ni mnyama ambaye ni mpole sana    Mnyenyekevu
  2. Hajichungi mwenyewepasipo mchungaji, anamtegemea mchungaji wake katika kupata majani
  3. Wakati anakatwa manyoa yake huwa hasumbui wala hajigusi

Sifa hizi ndizo zilifanya Bwana Yesu afananishwe na kondoo, tofauti na wanyama wengine ambao sifa zao huwa si nzuri sana mfano mbuzi, huyu ni mnyama ambaye ni jeuri, hana utulivu nk.. ndiyo maana Bwana hakufananishwa naye kabisa

Ndiyo maana baadhi ya maandiko yamentaja Yesu Kristo ni mpole

Mathayo 21:5 “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.

Wakati mwingine alijitambulisha mwenyewe kuwa ni mpole

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; KWA KUWA MIMI NI MPOLE na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

YESU KRISTO alikuja duniani ili tuwe na uzima tele ndiyo maana alikuja kwa sura ya mwana-kondoo, mpole na myenyekevu ili kumwita kila mmoja ili Kila mwanadamu apate kuifikia ile ahadi aliyoiweka mbele yetu

Ufunuo wa Yohana 3:20

[20]Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Usifanye moyo wako mgumu pale unaposikia sauti ya upole ikikuita mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *