“Mwenye haki akianguka mara saba ataondoka tena, nini maana ya mstari huu”?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe, karibu katika kujifunza tena

Mastari huu umekuwa ukitafsriwa tofauti, imekuwa ilidhahaniwa kuwa mstarii huu unamaanisha Mtakatifu kuanguka katika dhambi, la sivyo kwa sababu ingekuwa Kila wakati mwenye haki ananguka katika dhambi ya wizi kisha anainuka, alafu tena baada ya mda anaanguka, badae tena anaanguka, ni wazi kuwa itamfanya kupoteza nguvu ya kumtumikia Mungu ndani yake

Lakini maandiko yanaeleza vizuri jambo hili

Hapa aandiko yalikuwa yanaeleza juu ya watu, ambao wao kazi ya kubwa huwa ipo kwa ajili ya kuangusha watakatifu wa Mungu, kuwafanya wasiiendelee mbele, ndipo hapo hiafanya mapingo ya kuharibu, akidhani kuwa atamrudiaha nyuma, lakini huwa kinyume na mipango, badala yake yule mtu huinuka tena na kusonga mbele ndiyo maana ya andiko hilo

Mithali 24:15 Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;

16 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.

 

Ndiyo maana tukisoma hata habari za mitume wa Yesu, walipitia upinzani mwingi, katika  kupigwa, kushutumiwa pasipo sababu lakini zote hizo zilikuwa ni ila za adui kuwafanya wakatae taama katika kuifanya kazi ya Bwana, lakini tunaona siku zote walisonga mbele hawakujali watauwawa, watapigwa lakini walimwamini Mungu kuwa katika yote hayo watasimama

Hivyo hivyo nasi tunapoona tunapita katika kipindi cha kupigwa, kuachwa, kuumizwa kwa sababu ya wokovu isiwe sababu ya kufanya ukate tamaa bali dumu katika maombi na kumwaminj Mungu kuwa utasimama tena na utasonga mbele

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *