Ifahamu hatima yako.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima ya mwokozi wetu.

Kama Mkristo ni muhimu sana kutambua hatima yako ni nini katika Ukristo ulionao. Ukishindwa kutambua hatima yako ni nini utajikuta unakosa shabaha juu ya kile Mungu anachotaka kukiona kwako. Utaelekekeza matumaini na nguvu zako nyingi na muda wako mwingi katika sehemu isiyokuwa sahihi na bado wakati Mwingine usipate matokeo.

Watu wengi wamemwamini Yesu Kristo pengine kutokana na jinsi walivyohubiriwa(kusikia kawa watumishi waliowahubiria) inaweza ikachangia kwa namna moja au nyingine.. Kuna wengine wamehubiriwa injili Yesu Kristo wakaamini kwa kuambiwa Yesu Kristo atawabariki katika biashara zao, atarudisha heshima zao kwenye familia,atawapa maisha mazuri,Familia nzuri,pengine atawapa kazi nzuri na afya njema, atawaponya magonjwa nk.

Hivyo pengine wakaamini kwamba kweli nikiamini itakuwa hivyo  wanapoamini mawazo yao yote yanakuwa katika kile walichoambiwa au kusikia.

Ni kweli Yesu Kristo anaweza kufanya yote hayo na zaidi ya hapo anaweza kufanya katika maisha yetu na si kwamba ni mambo mabaya la! Ni mazuri ambayo kweli pia tunayahitaji katika maisha yetu.

Lakini sio kusudi kuu la  Yesu Kristo sisi kutufanya mabilionea, au wafanya biashara wakubwa au kuwa watu maarufu ulimwengu nk hilo sio kusudi kuu kabisa hayo yote ni mengineyo tu ambayo Kristo anaweza kutupa na zaidi.

Na hii inachangiwa pia na jinsi watu wanavyosikia injili kutoka kwa hao watu wanavyowahubiria kwa kuwaaminisha zaidi katika mambo ya mwilini tu kuliko mambo ya Rohoni.

Na watu wanaelekeza nguvu kubwa sana katika maombi yao na akili zao zinalalia(wanaabudu sanamu pasipo kujua) huko na mwisho mambo hayo yanapokawia inakuwa ni rahisi kuanza kupoteza tumaini nk.

Lakini hatima ya mwamini yaani jinsi Mungu anavyotaka kutuona sisi ni tofauti na jinsi tunavyofikiri. Mungu anataka kutuona sisi kila siku tunapiga hatua mwisho tunafikia ukamilifu.

Ni sawa na Mkulima anaepanda mbegu katika shamba lake ijapokuwa ile mbegu itapita katika hatua nyingi lakini mwisho wa siku mkulima yule anatazamia kuona kile alichokipanda kinatoa matunda na sio matunda tu ili mradi hapana! Bali matunda yanayofanana na kile alichokipanda.

Ikiwa alipanda mahindi hatarajii kuvuna mapera katika mahindi hayo la! Vivyo hivyo na sisi Mungu kuna hatima fulani ambayo anataka mwisho wa siku tuifikie.

Sasa ni hatima gani hiyo hebu tusome maandiko..

Warumi 8:29“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.”

Ukisoma kwa vizuri hapo katika mstari wa 29b anasema. “…Tangu asili WAFANANISHWE NA MFANO WA MWANA WAKE, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.”

Unaona hapo? Tumechaguliwa Tangu asili yaani kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu ili sisi tufanane na Yesu Kristo.

Hivyo hatima yako kama Mkristo ni wewe kufanana na Yesu Kristo kama vile Yesu Kristo alivyosema “aliemuona Yeye amemuona Baba” vivyo hivyo na sisi jambo hilo linatakiwa kuwa kwetu tuwe na ujasiri na uhakika ndani yetu wa wakuse.. “Ukiniona mimi umemuona Yesu Kristo” halaluya…! Tutaona ni kwa namna gani tunafana na Yesu Kristo katika mambo gani.. lakini maandiko bado yanatwambia.

1 Wakorintho 15:49“Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.”

Unaona hapo anasema. “… Kadhalika TUTAICHUKUA SURA YAKE YEYE ALIYE MBINGUNU.” hapa hamanishi nyuso zetu ziwe kama za Yesu katika mwili la! Bali ufahamu wetu,fikra zetu, kuenenda kwetu,kuongea kwetu,nk vyote vikamfananie kama jinsi Kristo alivyo.. Glory to God…

Maandiko yanaendelea kusema..

2 Wakorintho 3:18“Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.”

Unaona hapo katika Mstari wa 18b anasema. “….Tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo TOKA UTUKUFU HADI UTUKUFU.” hatutakiwi kubaki vile vile tu la!

Hivyo tunabadilishwa siku baada ya siku kutoka utukufu kwenda utukufu ili tumfananie Kristo katika kila kitu.. hatuwezi kuwa kama Kristo asilimia zote la! Lakini tunazidi kubadilishwa ili tufanane na yeye ndio maana anasema wakati mwingine “Mfano wake” maana ya mfano si kile kitu halisi lakini ni kitu kinachowakilisha uhalisia wa kitu fulani kwa karibu asilimia 70 % au 80% hakiwezi kuwa 100%.

Kama  wanafunzi waliokuwa Antiokia ambapo ndio jina Wakristo ndio lilipoanzia..

Matendo ya Mitume 11:26“hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.”

Unaona hapo! Hawa Wanafunzi Waliitwa wa Kristo kwa sababu ya watu waliona jinsi kuishi kwao,kutembea kwao,kuongea kwako,Mwenendo wao wate ulikuwa kama wa Yesu Kristo. Jinsi ambavyo walikuwa wanazidi kubadilika siku baada ya siku hakikuwa kitendo cha siku moja la!

Na sasa tunafanana na Kristo katika maeneo makuu saba ambayo moja baada ya jingine inatubidi kuliendea maandiko Mtume Petro anaelezea jambo hilo. Na mambo hayo yanatufanya kwenda utukufu hadi utukufu HALELUYA..!

2 Petro 1

5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,

6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,

7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.

Mambo haya saba yakiwa kwetu kwa wingi ni hakika tutakuwa ni kamaYesu Kristo duniani hapa wala hatutajikwa kabisa kwa Lolote ndani yetu.

Ndio maana Mtume Petro..

2 Petro 1

9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.

10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.

Mkristo anapokosa mambo kama hayo maadiko yanasema ni kipofu hawezi kuona vitu vilivyombali.. si kipofu wa Mwilini la bali wa rohoni.

Hivyo kama Mkristo Fahamu kabisa hatima yako wewe ni kufanana na Kristo. Sio kufanana na mchungaji wako,au mtu fulani yoyote duniani,wala sio kuwa billionea nk la! Bali ni wewe kufanana na Yesu Kristo. Kila siku piga hatua.

Kuwa na kiu na shauku ndani yako ya kufanana na Yeye kweli kweli unapoomba elekeza ufahamu wako wote kwa Mungu na kile unachokitamka mdomoni kiwe ni sawa sawa na kile unachokitamani katika moyo wako hakika mchakato huo utaanza ndani yako na siku baada ya utajikuta unafanana na Kristo Mwokozi.

Ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *