FAHAMU KWA NINI RAHELI ALIIBA VINYAGO(MIUNGU) YA BABA YAKE.

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Swali: kwa nini Raheli aliiba miungu ya baba yake? Je alitaka kwenda kuiabudu na wakati ni makosa mbele za Mungu.

Kabla ya kwenda moja kwa moja kulijibu swali hili tusome kwa ufupi kifungu hiki kidogo.

Mwanzo 31:18 “Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani.

19 Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye”.

Kusudi/lengo kubwa la Raheli kuviiba vinyago alivyokuwa anaviabudu baba yake si kwamba akaendelee kuviabudu bali lengo lake hakuwa anataka baba yake aendelee kuviabudu vinyago hivyo.

Alitaka kuviteketeza tutaliona hili mbele kidogo 

Maana mke aliekuwa wa ahadi wa Yakobo alikuwa ni Raheli na si Leah lakini Labani alimdamganya akampa Leah usiku ule..

Mwanzo 29:25 “Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda?

26 Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa”

Raheli aliona chanzo cha shida zote/Matatizo yote(ugomvi kati ya Yakobo na Labani ) ni hivyo vinyago.

Sasa ukiendelea kusoma zaidi utaona mambo ya ajabu ajabu ambayo Labani alikuwa anamfanyia Yakobo hata kutaka kumfilisi vitu vyake..

 

Mwanzo 31:36-42

36 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N’nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?

37 Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu.

38 Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo zako wala mbuzi zako wake hawakuharibu mimba wala waume katika wanyama wako sikuwala.

39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku.

40 Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu.

41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.

42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu”.

Sasa mambo mengi yalikuwa yanatokea Raheli alikuwa anaona yote na moja kwa moja akaona shida iko kwa Baba yake kutokaka na vinyago anavyoviabudu. Akajua hata Labani akimruhusu anyone anaweza akamfanyia mambo yasiyofaa..

Hivyo baada ya Yakobo kuondoka na wake zake wote Leah na Raheli. Mdogo mtu aliviiba vinyago vya baba yake ili visiendelee kumtawala na kumharibu zaidi akili yake na ndio maana akaondoka navyo ili kumsaidia baba yake..

Maana angeendelea kukaa navyo Labani asingelifika mbali angelikutana na ghadhabu ya Mungu na angelfish sehemu ambayo si sahihi maana maandiko yanasema waabudu sanamu hawataurithi ufalme wa Mungu.  Sehemu yao ni katika ziwa la moto.

Na ndio maana hata baada ya kufanya hivyo Raheli alivikalia vinyago vile. Angelikuwa na lengo la kuviabudu asingeweza kufanya vile maana asingeweza kumkalia mungu anaemsujudia. Maana wanaziheshimu sana kuliko kitu chochote.

Na tunaona baada ya hapo hatuoni tena Yakobo akifatiliwa na Labani.  Hiyo ikitufundisha pia sisi watu tuliomwamini Yesu Kristo kuna mazingira tutawaokoa watu kwa kuwanyakua kutoka kwenye hatari mbaya ambayo ingegharimu maisha yao kama vile tu Raheli alivyofanya kwa baba yake..

Maandiko yanasema…

Yuda 1:2 “na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”.

Ubarikiwe sana. 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *