Fahamu maana mstari huu “Tupa chakula chako usoni pa maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi”. (Mhubiri 11:1)

Maswali ya Biblia No Comments

Mhubiri 11:1

[1]Tupa chakula chako usoni pa maji;
Maana utakiona baada ya siku nyingi.

Mwandishi wa kitabu hiki,  alitumia neno tupa na si tunza au hifadhi lakini tunaona anasema tupa chakula chako usoni pa maji, hakuishia kusema tupa chakula chako lakini anaendelea kwa kusema hicho chakula akitupe baharini, kama tunavyojua kitu chochote kama kikitupwa kwenye maji yenye kina kirefu huwa kinapotelea huko huko, sasa sebuse chakula ambacho kama kikiloa maji kinayeyuka itakuwaje kama kikitupwa katika bahari kama mwandishi wa kitabu alivyosema…
Maana anasema baada ya kukitupa hicho chakula ndani ya maji atakiona baada ya siku nyingi

Jambo ambalo tunajifunza hapa katika Kifungu hiki, ni kuwa

(Mhubiri 11: 2 Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane; Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi

Maana halisi ya mstari huu, inagusia katika swala la utoji, na hapo alipozungumzia maji, au bahari aliwakilisha watu, au ulimwengu

Ufunuo wa Yohana 17:15
[15]Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.

Tunapojitoa kwa ajili ya wengine kwa sawa na kupata chakula bahari, japo kwa ule tunapofanya vile tunaona kama tunapoteza lakini mbele za Mungu ni kitu kikunwa sana ambacho kinafanyika, ndiyo maana maandiko yanamalizia kwa akusema utakiona baada ya siku nyingi, kumbe yale tunayofanya kwa ajili ya wengine, mwisho wa siku tunalipwa

Usione kama unapoteza unapojitoa kwa mali zako, mda wako nk. Kwa ajili ya Bwana jua kabisa kile unachokifanya baadae utapata malipo yake, hivyo usichoke kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana

Ubarikiwe..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *