Maana ya kalibu ni TANURU, pale mazingira yanaposafishwa mara nyingi zile nyasi au takataka huchukuliwa kisha hupelekwa kuchomwa moto, sasa hicho kitendo cha kuchukua majani na kwenda kuyateketeza katika moto hiyo sehemu ndiyo inaitwa kalibuni yaani “TANURU”
Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?”
Jambo hili Mungu alilisema kutuonyesha namna anavyomthamini mwanadamu kuliko hata majani ya kondeni, japo nayo huyatunza na kuyavika, hata yakitazamwa huvutia machoni pa wanadamu, lakini kesho kidogo tu hutupwa kalibuni yaani kwenye ( TANURU)
Hivyo Mungu alitaka kutujilisha kuwa sisi ni zaidi ya hayo maua kama anayavisha, sasa sisi ni zaidi hutuvisha zaidi , kama ni chakula anayapa basi sisi zaidi hutuoa chakula zaidi na zaidi, kiuhalisia ni kuwa Mungu amempa mwanadamu uthamani au upendeleo mkubwa zaidi kuliko viumbe vyote
Ndiyo maana anasema katika
Mathayo 6:30-34
[30]Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?[31]Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Mungu anachokihitaji kutoka kwetu wanadamu tuutafute ufalme wake kwanza na haki yake na hayo mengine atatupa atatuzidishia, si kwanza tusifanye kazi hapana bali hizo kazi za mikono zisichukue uthamani wa Mungu maishani mwako hata ikapelekea kutengemea kutumia akili zako kuliko kumtegemea Mungu,
MAISHA YAKO YOTE MUWEKE MUNGU KUWA NAMBA MOJA, Unapotembea, unapolala, unapofanya shughuli zako katika hali zote MUNGU NI KWANZA
Maran atha
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.