Fahamu maana ya kuota mbwa

Ndoto No Comments

Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo Bwana wetu. Karibu Tuyatafakari pamoja maneno ya Uzima.

Mbwa kiroho huwakilisha vitu mbalimbali. Sasa inategemea sana na ndoto imekuja katika mazingira Gani na uzito upi (kujirudia rudia). Mbwa anaweza wakilisha mlinzi, adui, au kitu Najisi {kichafu}. Sasa tuchambue hizi ishara tatu kwa ufupi

1. MBWA KAMA MLINZI

Sifa mojawapo ya Mbwa ni ulinzi, na watumishi wa Mungu pia hufananishwa nabwa mlinzi, na wale wasiosimama katika nafasi kikamilifu hufananishwa na Mbwa wasiobweka Wala kung’ata

Isaya 56:9-11

9 “Enyi hayawani wote wa nyikani, njoni, Mle, enyi hayawani wote wa mwituni.

10 Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni MBWA WALIO BUBU, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.

11 Naam, MBWA HAO wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.”

Ukiota Mbwa huyu amesimama getini anafukuza kitu, ama anafanya Jambo Fulani kwa ujasiri pasipo  madhara yoyote kwako basi ni Ujumbe kutoka kwa Mungu kwamba uzidi kusimama katika nafasi yako kama mlinzi.

Lakini, ikiwa Mbwa huyo ni mwoga, anayekimbizwa kimbizwa, Basi hizo ndio nguvu zako Rohoni. Unapaswa utengeneze na Mungu wako maana anakuona si mkamilifu katika Utumishi wako.

2. MBWA KAMA ADUI.

Tusome..

Zaburi 22:16

” Kwa maana MBWA wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu.”

Zaburi 22:20

“Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za MBWA.”

Sasa unapoota aidha unakimbizwa, unaviziwa, unatishwa, umezungukwa ama kushambuliwa na Mbwa, basi hizo ni vita za kiroho.Ibilisi anataka kuiba kilicho chako Au kukuangamiza kabisa.

Ukiwa kama mwamini inakupasa uongeze Maombi zaidi, Ongeza kumtumikia Bwana maana ni ngao kubwa sana, ukimsihi Bwana akulinde mbali na mashambulizi hayo ya Adui.

Wafilipi 3:2

“Jihadharini na MBWA, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.”

Ikiwa bado hujaokoka basi Mrudie Mungu wako hivi Leo, La sivyo! Utakuwa hatarini Kuangamizwa kabisa na Adui.

3. MBWA KAMA KITU NAJISI

Mbwa kibiblia anawakilisha unajisi au uchafu maana hajali anakula Nini anaweza rudia hata matapishi yake ( soma mithali 26:11)

Ni wanyama wasiostahili Heshima yoyote

Mathayo 15:26 ” Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

Katika swala la kupata watoto Mbwa hushiriki na yeyote bila kujali hata awe mama yake, hivyo huwakilisha Uovu, watu Waovu wasiojali kabisa maisha yao ya kiroho.

Ikiwa unawaota mara kwa mara Mbwa usiowaelewa lengo lao, Leo wapo hivi kesho vile, Naam ndivyo Mungu akuonavyo.

Tubu dhambi zako mgeukie Mungu Leo, kama upo katika Hali hiyo, kumbuka hatma ya watu wa namna hiyo ni kuzimu. Biblia inasisitiza kwa walio hivyo Rohoni

Ufunuo wa Yohana 22:15 “Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.”

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *