Fahamu maana ya Mithali 27:10.

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo.

Andiko hili linamaanisha nini kusema“usimuache rafiki yako wala rafiki ya baba yako….”

Tusome mstari huu…

Mithali 27:10 “Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.

Andiko hili linatufundisha umuhimu wa marafiki wema(ambao ni kama ndugu wa damu nk)

Sasa mstari huu unaanza kwa kusema “usimuache rafiki yako mwenyewe wala rafiki ya baba yako…” kwa sababu watu/marafiki hawa wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako wakati wa taabu au wakati utakapohitaji msaada wa haraka.

Hivyo si kwamba ndugu hawawezi kuwa ni msaada mkubwa kwako la! Bali kama tukiwatumainia ndugu tu ni wazi kuna mambo hayataenda..

Mfano ndugu zako wako mkoani na umepata ajali na kuumia ni wazi kuwa ikiwa uko dar es salaam na ndugu zako wako mikoani ni ngumu sana wakatoka mkoani kwa wakati huo huo na kuja kukupa msaada bali watu wako wa karibu..yaani marafiki ndio watakaokuwa wa kwanza kabisa kukutembelea na kukutia moyo.

Hivyo mstari huu unatusisitiza zaidi sana kutokuwapuuza marafiki hata wa ndugu zetu au marafiki zetu wenyewe.

Na Tafsiri ya Rafiki ni mtu ambae anajitoa kwa ajili yako katika hali zote katika shida na katika raha pia.

Hivyo ikiwa ni rafiki wa baba yako,mama yako,kaka/dada yako usimpuuze hata kidogo maana hao watakuwa ni msaada bora na wakaribu pale utakapohitaji msaada.

Sasa tunapomwamini Yesu Kristo tunapata marafiki ambao ni bora na hawa ni zaidi hata ya ndugu wa damu. Ambao watajitoa kukuombea nk pale unapokuwa katika changamoto fulani ama ukiwa huna changamoto ndugu katika Kristo wanakuwa na wewe wakati wowote na majira yote..

Hivyo ndugu tulionao katika Kristo ni wa muhimu sana sana wala usiwapuuze na kuimarisha urafiki na watu wa kidunia ilihali umeokoka hivyo imarisha urafiki wako na ndugu walio katika Kristo Yesu..

Na ndio maana hata katika mstari huo anamalizia kwa kusema “…Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.”

Ikiwa na maana pia ndugu aliembari katika jambo linalohitaji utatuzi wa haraka basi anaweza asikufaidie kwa lolote ila jirani yupo na wewe wakati wote ambae anaweza kukusaidia.

Hivyo ndugu katika Kristo Yesu ni bora zaidi kushinda hata ndugu/marafiki wa kidunia. Tafuta kuimarisha mahusiano yako vizuri  na marafiki (watu waliookoka) usiwakimbie..

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *