Fahamu maana ya mstari huu waefeso 3:15 “Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.”

Maswali ya Biblia No Comments

Tunachopaswa kufahamu ni kuwa “Mungu ni BABA wa kila kitu hapa duniani na mbinguni pia, ndiyo maana Paulo akasema maneno haya

Waefeso 3:14 “Kwa hiyo nampigia Baba magoti,

15 ambaye kwa jina lake UBABA WOTE WA MBINGUNI NA WA DUNIANI UNAITWA”,

Kama ilivyo wajibu wa baba wa kimwili ulivyo katika familia yake, jinsi anavyojali, navyohudumia, anavyotekeleza mahitaji kwa Kila mtu, sasa hivyo hivyo kwa Mungu wetu ni zaidi maana yeye hutoa mahitaji kwa wanadamu pamoja na kwa malaika hivyo yeye ni baba ambaye anapaswa kuabududiwa na kusujudiwa

Wakolosai 1:16 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake”.

Na wewe ambaye tayari umemwami Bwana wetu Yesu Kristo hatupaswi kuogopa Wala kuona shaka, maana tuliye naye na BABA nauejali kutoka kwetu na kuingia kwetu hivyo usikate tamaa kumbuka BABA anajua mahitaji yako yote, zidi kusonga mbele na kuwashuhudia wengine kuwa Bwana Yesu pekee anapaswa kuabudiwa

Wafilipi 2:9 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *