Fahamu maana ya mzushi kibiblia

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa muumba wetu.

MZUSHI NI NANI?

Ni mtu anayezusha au kuolongea jambo ambalo lina makusudio ya kuweka mgawanyiko.

Hata katika kanisa wapo wazushi wanaozusha mambo ili kuleta mgawanyiko katika kanisa.

Biblia imesema tusiwape nafasi wazushi.

Tito 3:10 inasema”mtu aliye mzushi baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili,i mkatae;

11 “ukijua ya kuwa MTU kama huyo amepotoka, Tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe”

Mfano wa mada zinazoleta mgawanyiko katika kanisa ni hizi.

Tito 3:9 “ lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya Sheria.kwakuwa hayana faida, Tena hayana maana”

  • Mashindano hayo yanaleta kiburi na mashindano katika kanisa.

Kwasababu ndani ya kanisa Kuna ambao ni wachanga kiroho ikiwa watasikia hayo mashindano baina ya watu na watu ndani ya kanisa itapelekea waiache Imani.

2timotheo 2:14 inasema” uwakumbushe mambo hayo, ukiwao ya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, Bali huwaharibu wasikiao,

1timotheo 6:4 inasema ”Amejivuna;Wala hafahamu neno lolote;Bali anawazimu wa kuwazia habari za maswali na madhindano ya maneno,ambayo katika hayo hutoka husuda,na magomvi na matukano,na shuku mbaya.

Na sisi katika kanisa inatupasa kuwa watu wa kujiepusha na uzushi na ikiwa wapo wazushi katika kanisa walioonywa zaidi ya mara mbili na hawabadiliki inatupasa kujiepusha nao ili tuutunze utakatifu wetu.

Kwa maoni na ushauri wasiliana nasi kwa namba hizi.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *