Fahamu maana ya vifungeni viuno vya nia zenu

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mpendwa karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana Yesu.

Tusome maandiko haya.

1Petro 1:13 “Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.

14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu”.

Popote inapozungumziwa katika biblia “kujifunga viuno” inamaanisha kuwa na utayari kipindi ambacho Wana wa Israeli walitolewa misri siku ya kwanza walipokuwa wakimla yule pasaka Bwana mungu aliwaambia wamle wakiwa wamevaa viatu miguuni, na kujifunga mkanda kiunoni maana yake(wawe katika mazingira ya kuondoka) na siuo mazingira ya kulala baada ya kula.

Kutoka 12:10 ‘Wala msisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.

11 Tena mtamla hivi; MTAKUWA MMEFUNGWA VIUNO VYENU, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana”.

Tunaposema” tujifunge viuno vya akili zetu” inamaana “tuwe tayari kiakili” pia “tujifunge viuno vya roho zetu” inamaana “tujiweke tayari katika roho zetu katika kumngojea Bwana” Bwana alisema katika Luka 12:35 neno linasema.

Luka 12:35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;

36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.

37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia”.

Anaposema “tujifunge viuno vya Nia zetu” anamaanisha “tujiweke tayari nia zetu” kwa mambo yanayofuata.

Hivyo 1petro 1:13 inamaana badala ya kusema “vifunge viuno vya nia zenu” unaweza kusema “kuweni tayari katika Nia zenu” kwa utimilifu wa Neema mtakayoletewa katika ufunuo wa yesu kristo. Neno linasema.

2Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;

2 lihubiri neno, UWE TAYARI, WAKATI UKUFAAO NA WAKATI USIOKUFAA, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”.

Siku za mwisho kristo anarudi na ujira wa Kila mmoja.neno linasema

Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *