fahamu tofauti ya kuhukumu na kulaumu

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Mwokozi wetu libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno la Mungu litupalo uzima wa maisha yetu

Ukisoma katika,

Luka 6:37 “Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa”.

Hapa tunaona neno la Mungu linatuqgiza kwa Habari ya kutokuhukumu Wala kulaumu, sasa je ni dhambi au makosa kumwambia mtu ukweli unapoona amefanya jambo isivyo stahili.

Jibu: maana ya Neno HUKUMU linamaanisha kutoa hatma ya moja kwa moja kwa mtu mwingine, na hii hutokea pale mmoja anapojiona kuwa yeye ni bora kuliko mwenzake , mfano anapoona mlevi, au mvuta bangi, au kahaba kisha akaanza kusema wewe ni “mtoto wa ibilisi kabisa” mwisho wako ni katika ziwa la moto tu, wewe umeshindika huwezi kwenda popote sasa kauli kama hizi Moja kwa Moja anakuwa tayari ametoa hukumu kwa hao watu, kwa sababu amezungumza maneno hayo tu pasipo kusema neno lolote ambalo lingine wajenga hiyo ndiyo maana halisi ya HUKUMU

KULAUMU ni kitendo cha kukosoa jambo, mfano unakuta kiongozi katoa kazi kwa watu fulani, sasa katika kuwasilishwa anakuta amefanyika tofauti na yeye alivyotaka, hapo hapo anaanza kukosoa, anaweza kusema ni Bora ingekuwa hivi au mngefanya hivi, sasa jambo hili moja kwa moja ni lawama, kwa sababu huyo kiongizi amejiona kuwa yeye anajua zaidi kuliko hao watu au mfano imetokea mtu ajitimiziwa jambo ambalo alikuwa analihitaji ambalo kweli lilikuwa la muhimu lakini kwa sababu kaona halijatimizwa kwa wakati hapo hapo anaza kulaumu yaani kumkosoa huyu mtu.

Sasa mambo haya yote mambo yote haya mawili mbele za Mungu ni machukizo wala Mungu hafurahishwi nayo, kwa sababu ukiangalia hata sisi kuwa hivi tulivyo Leo tunamuelewa Mungu, tunaweza kuishia kulingana na neno lake, hatukupata haya kwa kuhukumiwa na kulaumiwa bali alitueleza kwa upole na kwa upendo hadi tukajikuta tumeamza kupenda kuisha maisha matakatifu.

Jambo lingine pia tunalopaswa kujua ni kuwa mfano pale mtu anapoenda kueleza mfano ameakutana na kahaba na akaanza kumueleza kuwa jambo ambalo analifanya ni machukizo mbele za Mungu, Wala si mapenzi ya Mungu kwa sababu si agizo lake na mwisho wake ni jehanaum, hapo anakuwa ajahuku bali amemuelezea ukweli wa jambo analolifabya na jinsi mwisho wake utakavyo kuwa…

Hivyo basi tusiwe watu wa kuhukumu watu Moja kwa Moja au kulaumu, bali tunapaswa tutoa fundisho juu ya kile wanachokifanya kuliko kuhukumu au kulaumu bila kuelekeza inapaswa kuwaje, na wewe utakaye sikia maonyo basi kibari kubadilika ukijua kabisa hauonewi bali unapendwa na Bwana anakusudi na wewe, usifatishe namna ya ulimwengu huu maana unapita …

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *