HATARI YA KUVAA SURUALI KWA MWANAMKE
Jina la Yesu Kristo Mfalme wa utukufu libarikiwe daima. Karibu tujifunze Biblia mwanga wa njia zetu.
Mbali na kuwa vazi la suruali kwa mwanamke ni machukizo mbele za Mungu sawa sawa na kumbukumbu 22:5, Lakini leo nataka ufahamu hatari nyingine ya kuvaa suruali.
Na hatari yenyewe ni kukaribisha maroho ndani yako ikiwemo majini makahaba, ni vizuri we kama mwanamke kufahamu hili ili utoke katika kifungo cha ibilisi, unapovaa suruali pasipo kujalisha ni pana kiasi gani maadam ni suruali.. katika ulimwengu wa roho unaonekana mwanaume, hivyo ile roho ya kiume itakuvaa tu, na hapo ndipo unajiukuta upo na mwanaume usiyemjua unalala naye kwenye ndoto, hayo ni mapepo/majini makahaba.
Wanawake wote wanaovaa suruali ni lazima tu wanasumbuliwa na hayo maroho kwenye ndoto, we mwenyewe kama ni mwanamke unayevaa masuruali utakuwa unafahamu hili. Hivyo suruali kwa mwanamke ni ajenda ya kishetani kabisa iliyobuniwa kuwapeleka wanawake kuzimu na kuwafanya wakose mbingu.
Mwanamke unapovaa suruali na kutembea njiani, tayari unazini na wanaume wanaokutamani..kwa maana mandiko yanasema ”amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake ” (Mathayo 5:28)..utaachaje kuota ndoto za uzinzi, wale wanaume wote waliokutamani usiku utakua nao tu..kwa ufupi kuvaa suruali ni kufungua mlango wa maroho ndani yako, ambayo matokeo yake ni kuwa mtumwa wa dhambi na mwisho kuishia jehanum ya moto. Na huo ni mpango wa shetani sio mpango wa Mungu, na wakulaumiwa ni wewe sio shetani kwasababu wewe ndiye umekubali kumkaribisha shetani kupitia hizo suruali na vimini pamoja na mambo mengine yote mabaya unayoyafanya.
Sasa suluhisho pekee la kutoka kwenye vifungo hivyo vya ibilisi sio kuombewa tu, bali ni wewe kusikia ujumbe huu na kutii wito wa Mungu kwa kutubu. Yaani unaamua kuachana na huo uvaaji wa kishetani, unazichoma moto hizo suruali zote na vimini, na kuondoa mapambo yote kwenye mwili wako, unaondoa hayo mawigi, hereni hata kama umenunua kwa gharama kubwa, unaviondoa vyote maana huo ni mlango wa mapepo ndani yako. Baada ya hapo nenda kabatizwe kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa jina la Bwana YESU ili ukazike kabisa kazi zote za ibilisi…na ukifanya hivyo kwa kumaniasha kabisa, Mungu atakupa Roho wake ambaye atakusaidia kuishi maisha ya utakatifu kirahisi sana.
Kumbuka wanawake wote waliokufa na masuruali na mapambo..hivi sasa wapo kuzimu wanajuta sana. Hebu fanya maamuzi mpe Yesu maisha yako leo usije ukajikuta kwenye majuto ya milele.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.