Ipi tofauti kati ya mwivi na mwizi?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, karibu tujifunze biblia,

JIBU
Mwivi na mwizi ni neno moja lenye maana ileile ila ni lugha mbili ambazo zipo katika nyakati mbili tofauti.

Biblia imetafsiriwa kwa kiswahili cha zamani kilichoitwa ‘kimvita’ ambacho kina maneno yasiyokuwepo kwa sasa kama vile mwivi na wevi yakimaanisha mwizi na wezi. Hiyo ndiyo sababu hatuwezi kuona neno mwizi na badala yake ni mwivi (Soma Kutoka 22:2, Ayubu 24:14, Zaburi 50:18, Mithali 6:30, Yoei 2:9, Luka 12:39)

Baadhi ya maneno mengine ya kimvita (kiswahili cha zamani) ambayo mengi hayatumiki kwa sasa ni jimbi badala ya jogoo, kiza badala ya giza, nyuni badala ya ndege, kongwa badala ya nira.

Hivyo basi neno mwivi na mwizi ni neno moja na lenye maana moja yaani mtu aliyeiba..

Lakini pia biblia inatuambia Yesu atakuja kama mwivi, yakupasa ujiandae kwa hilo..

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”

Maran atha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *