Je kandake ni nini?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima kutoka kwa Bwana wetu yesu kristo.

Filipo mhubiri wa injili aliagizwa na malaika wa Bwana aende njia ya jangwani ( Gaza) alipokuwa akielekea huko njiani alikutana na mkushi ( towashi) ili akamhubiria  injili na siku hiyo akabatizwa na kupelekwa eneo lingine.tukisoma maneno ya uzima yanasema.

Matendo 8:26 “Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.

27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu”

Mkushi alikuwa na mamlaka juu ya kandake yaani malkia wa nchi ya kushi ambapo kandake ni cheo.

Towashi aliye wekwa chini ya umalkia huo ili kuitunza hazina yote ya kushi ilikuwa ni desturi za kifalme nyingi za zamani pindi wanapotaka kuweka chini malkia wao hususani kwenye sekta za fedha waliwaasi watumwa wao ili wasiwe na tamaa za mwili wafikirie kuacha utumwa wao na kujali familia zao pia iliwafanya wawe wanyenyekevu na makini sana.

Inatufundisha tukuwekwa chini ya kazi ya Mungu inategemea uaminifu wetu na rohoni tunatakiwa tuwe kama matowashi tufe katika habari za ulimwengu na tamaa ili tukijaribiwa kwa mali, uzinzi n.k Bali unabaki kuwa ni yuleyule ambaye haujabadilishwa na namna za Dania.

Mungu anatamani tuufikie utakatifu wa kutokubadilishwa tabia,mienendo n.k ili tufanane na matowashi NDANI ya mioyo yetu kama Ayubu anasema katika Ayubu 31:1,25

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *