Je kujihusisha na michezo ni dhambi ?

Maswali ya Biblia No Comments

Swali: Je kujihusisha na michezo mfano kushabikia Mpira au kushabikia timu fulani ni makosa

Jibu: Neno la Mungu linasema, tusome

Wafilipi 2: 3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake’’

Yaani jambo lolote lile ambalo kama likifanyika na kupelekea malumbano kishindana nk.. mbele za Mungu ni makosa, kulingana na swali hapo kwanza kabisa lazima tujue kuwa kimuingiacho mtu si najisi bali kimtokacho mtu ndiyo najisi

Kwa namna gani sasa mtu anapoangali Mpira au kushabikia timu fulani, pale anapokuwa akiangalia hakiweki kumpa madhara yeyote lakini madhara yanakuja pale anapoanza kukitoa nje hicho kilichoingia ndani yake ndiyo hapo utaona matokea yaanza hapo maneno mabaya yatanza kutoka, mashindano, ugomvi sasa haya ndiyo mambo ambayo yanamtia mtu unajisi , kwahiyo Moja kwa Moja jambo hili ni baya neno la Mungu linasema

Wafilipi 2: 14 ‘’Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,

15 mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu’’.

Jiulize pia umepata faida gani tangu uanze kushabikia Mpira, je hizo dakika tisini zimeleta matokeo gani kwako, je baada ya kuleta mashindano, je umewaokoka wangapi kutoka katika dhambi, ukiona kuwa hakuna faida ayeyeotw uliyoipata jua kabisa jambo unalokifanya ni baya machoni pa Mungu.

Badili mtazamo wako Leo, ikiwa kama ulikuwa unaweza kukaa dakika tisini bila kusinzia, basi nguvu hiyo wekeza katika Bwana, hakikisha usinzia pia ukiwa ibadani, kwenye mkesha na mambo yote yanayohusiana na Mungu, anza kutangaza Habari njema katika kinywa chako acha na mambo ya ulimwengu huu, kumbuka mambo yote yatapita lakini neno la Mungu litadumu milele.

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *