Bwana Yesu asifiwe karibu katika kujifunza Neno la Mungu .
Mathayo 16:24
[24]Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Kujikana ambako Bwana Yesu alikuwa anakuzungimzia ni kukataa matamanio yako, maana ya Neno lenyewe kujikana ni kukataa matamanio yako au mipango yako na kuielekeza sehemu nyingine.., ila kibilia kujikana inamaanisha kujikana mbele za Bwana wetu Yesu Kristo, pale upoamua kumpa Yesu Kristo maisha yako ili ayaongoze hapo unakuwa umejikana hapo sasa ndiyo unaacha mambo ambayo ulikuwa unayafanya na kumgeukia yeye
Hapa unaanza kubadilika kimwenendo kwa mambo yote ambayo ulikuwa unayafanya ambayo yalikuwa ni machukizo mbele za Mungu unanza kuyaacha hata kama yalikuwa yanakupa faida kiasi gani yote unayaacha, mfano kwa kijana wa kiume mfano ulikuwa uvaa vibaya, una makundi mabaya, au unafanya kazi haramu nk. Pale unapoamua kuyaacha na kumfata Kristo huko ndiko kujikana, na kwa Binti vivyo hivyo nawe ikiwa kuna vitu ulikuwa unavipenda, kuvaa vimini, suluari, kujibadili rangi nk..vyote hivyo unaanza kuviona si kitu maana tayari Kristo yupo ndani yako“
wafilipi 3:7
Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.
8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;
Maisha ya Kila mtu hapa Dunia, kwa Kila mmoja tunapaswa kijikana nafsi zetu, kuachana na mambo ya ulimwengu huu na kufata kile ambacho Mungu ametuagiza kutifanye, na ikiwa tayari umekoka lakini Bado kuna baadhi ya mambo Bado unayafanya basi ni muhimu kuyaacha ila usimtumikie Mungu katika unafiki..
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.