Je! Ni kweli isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Turejee maandiko haya

Mwanzo 24:67 “Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake”.

Isaka alikuwa ni mwana pekee kwa mama yake, kwahiyo  hili andiko halikumaanisha kuwa  isaka alipenda na kukifurahia kifo cha mamaye bali alipata faraja kutoka kwa Rebeka mkewe ambaye alikuwa akimfariji kama mama yake hii ikapelekea kuona faraja kwa sehemu ambayo iliondoa Hali ya huzuni na upweke ndani ya moyo wake isaka.

Lipo jambo la kujifunza kwa wanawake

Hapa wanawake wanapewa namna bora ya kuishi na waume zao, siku zote mwanamke unapasa ufanyike kuwa faraja na tulizo kwa mme wako, tena pale ambapo wanapatwa na matatizo zaidi ya msiba lakini pia hata wakati wa baraka wanapaswa kuwa bega kwa bega na huo ndiyo upendo wa kweli na upendo huu unatoka pekee kwa mume au mke sahihi kutoka kwa Bwana.

Pia ukitaka kupata mke au mume Bora inatupasa umuombe Bwa naye atakupatia hitaji la mioyo yetu

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *