Je sala ya mtakatifu Ritta kashia ni sahihi?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom,karibu tujifunze Neno la Mungu

Mtakatifu Ritta ambaye kwa kanisa katoliki anajulikana kama mwombezi wa mambo yasiyowezekana, mfanya miujiza..

Mama huyu alizaliwa 1381 Katika mji unaoitwa kashia kwenye taifa la Italy, mama huyu aliolewa akiwa mwenye umri mdogo, lakini alikuja kufiwa na mume wake na Watoto wake wawili ndipo akajiunga na utawa, ingawaje alipitia changamoto nyingi kujiunga kwasababu alikuwa ameshaolewa, sio bikira) pamoja na changamoto zote ila alifanikiwa kujiunga..

Kutokana na imani ya kikatoliki kupitia mama huyu Maombi yake yaliwaletea majibu wengi, na utambulisho mwingine aliokuwa nao ni jeraha ndogo kwenye paji la uso wake, wakiwa na imani kuwa ni alama ya kuwa mKristo kufuatia mateso ya  Bwana Yesu msalabani, pale alipowekewa taji ya miiba, aliondoka duniani,(kufa) kati ya umri wa miaka 75_76,

Ilipofika tarehe 24 may 1990,papa leo X111 alimtangaza mama huyu ni Mtakatifu, kwa kanisa katoliki ukitangazwa kuwa Mtakatifu maana yake umekidhi vigezo vya kuwaombea walio hai,

Toka kipindi hicho wakatoliki wamekuwa wakifanya novena na kumsalia litania, na wengi wakishuhudia kuwa matatizo yao sugu yakitatulika, na hiyo ikamfanya kuwa maarufu sana,

Jambo hili lina uhalisia wowote?

Ni lazima tuyafahamu maandiko yanasema nini,maana yake yatupasa kuwa wasomaji sana, kwenye biblia hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kwamba watakatifu wa zamani au sasa wanaweza kutuombea au kutufanyia maombi, zaidi sana biblia imeelezea kwamba hawajui Chochote kinachoendelea duniani..

Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Umesoma hapo,

Kwa ufupi desturi hii ya kupeleka maombi yetu kwa watakatifu waliokufa ili watuombee ni yakipagani, hizi ndizo ibada za sanamu, chimbuko lake lilianzia kwenye hizi dini zinazoamini mizimu inaweza kuzungumza na wanadamu, tunapoyasema haya,hatuna maana tunachuki na ukatoliki au watu wao wala kupinga bali lazima ukweli usemwe ili wote tuweze kupona kwa kuwa njia yetu ni moja na lengo ni ili wote tuurithi uzima wa milele aliotupa Bwana Yesu..

Usipumbazwe ukaona novena ya Ritta ilikuletea majibu kiasi gani, hiyo tayari ni ibada za sanamu, kwasababu hata shetani naye anaweza kukupa majibu, usione ajabu kupokea majibu hayo kumbe lengo ni ili upumbazike.

2Wakorintho 11:14  Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Anayetuombea sisi, mwombezi wa watu wote ni mmoja tu ,ndiye YESU KRISTO MWOKOZI (1Yohana 2:1).,sio paulo, petro, Mariamu au yusufu, hawa wote waliitaji kukombolewa kama sisi tu,, kwa pamoja wote walituelekeza kumfata Bwana Yesu, na sio wao,

Mtume Paulo alisema hivi..

1Wakorintho 1:13  Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Huna haja ya kupeleka maombi kwa watakatifu waliokufa kwasababu na hao pia hawawezi kutuombea sisi, wewe pia huwezi kumuombea mwenye dhambi Bwana amtoe kwenye mateso, imani kama hizi haipo kwenye biblia, Soma (Waebrania 9:27). Fundisho la mtu kupitia toharani halipo kabisa kwenye maandiko..

Kuwa mtu wa kusoma neno la Mungu, utayafahamu mengi, tutaishi kwa neno la Mungu na sio mapokeo ya kidini, unaweza kuwashangaa na kuwadharau wanaoabudu mawe lakini na wewe ukawa mmoja wapo kwasababu wewe upo tu kwenye mfumo mwingine, ukimruhusu Roho Mtakatifu akufundishe maandiko utajikuta unafunguka katika mengi na kukataa kuwa mfuasi wa kidini..

Kama ulikuwa ni mojawapo wa waliokuwa wakipeleka maomb yao kwa Mtakatifu Rita wa kashia, au Mtakatifu mwingine tofauti, kuanzia sasa ACHA kabisa, na utubu dhambi zako, ubatizwe na kupokea Roho Mtakatifu, yeye atakuongoza kwenye kweli yote,(Yohana 16:13

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *