Je shetani ni mzuri wa sura au ana mapembe?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu mpendwa katika Bwana tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana wetu yesu kristo.

Shetani ni nani? shetani ni malaika aliyetupwa kutoka mbinguni Hadi duniani baada ya kumuasi Bwana Mungu.

Japo! duniani Kuna udanganyifu mkubwa ambapo watu wanadhani kuwa shetani anazo pembe za kutisha, anaishi maeneo ya makaburini na wengine hudhania ya kuwa shetani ni kitu cha kutisha lakini hawajui kuwa alikuwa malaika lakini baada ya kuasi alishushwa na kuwa shetani.

Hivyo baada ya kuanguka kwake aligeuka na kuwa mshitaki wetu mbele za Bwana na biblia inaposema kuwa amelaaniwa haimaanishi kwamba amelaaniw kimaumbile Bali katika rohoni.

Mwanadamu akikosea huwa anabadilishwa na kuwa kitu cha kutisha ambapo ni kwenye  roho, maana ndiyo huwa inabadilishwa.

Vivyo hivyo hata kwa shetani na malaika zake wanao uwezo wa kujibadilisha wapendavyo hata kujifanya kama malaika wa Nuru hawajsondolewa ujuzi wao wrote waliokuwa nao isipokuwa hawana uwezo wowote wa kumshinda mtu aliye ndani ya kristo.ukisoma

2Wakorintho 11:3 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.

14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

Hawa watu wote ni waasi pamoja na viumbe vilivyoasi wapo tu kama walivyoumbwa isipokuwa tabia zao ndizo zinazowatofautisha kwakuwa tayari wameshalaaniwa wakingojea mauti ya pili ya like ziwa la moto.

Hivyo vita unayopigana ni vita ya malaika na vita kubwa iliyopo ni kukufanya uiache Imani yako na usiende mbinguni hivyo inatapasa kuwa imara wito wetu kwakuwa ni kama simba angurumaye.kama inavyosemwa katika

1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

Barikiwa sana

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *