Bwana Yesu asifiwe karibu katika kujifunza Neno la Mungu
Swali: “Kama Mungu alituumba yeye kwanini siku ya mwisho awachome watu katika ziwa la moto”?
JIBU: Kwanza kabisa kitu ambacho tunapaswa kukitambua kwa Mungu wetu, sifa yake kuu yeye ni UPENDO, tena mwingi Rehema, na upendo wake hauchangui mwema au mbaya katika kupenda yeye anapenda kila mtu, tena ni Mungu ambaye yupo na uvumilivu sana, anamvumilia kila mtu ili aache njia yake mbaya na kumfuta yeye japo anafanya mabaya lakini Mungu Uvumilia tu akijua kuwa utabadilika , na Mungu hamkomoi mtu yoyote bali ni Mungu mwenye Upendo na Uvumilivu
Warumi 2:4
[4]Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na Uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
Umeona hapo japo wanadamu tunafanya mabaya lakini kumbe Mungu anatuvulimia nasi katika ili tupate kutubu.
Sasa tukirudika katika swali letu, ukweli ni kwamba Mungu wetu ni mwingi wa Rehema tena ni mvumiluvu sana, lakini anayo pia sifa yake kuu ambayo anamtambulisha Sifa nyingine ya Mungu ni UTAKATIFU, (usafi au ukamilifu wa jambo fulani)
1 Petro 15: 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.
17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
Sasa ikiwa yeye ni Mtakatifu ( msafi ) ni wazi kabisa hawezi kuchangamana na uchafu, ndiyo maana maandiko yanasema “afichaye dhambi zake hatasamehewa”, hii ikituongoza kuwa njia ya kuondoka uchafu ili tuweze kuwa kama Mungu na tuweze kuepuka gadhabu zake ni kutoficha dhambi, bali kuziweka wazi ili tuwe watakatifu kama Mungu wetu, mfano mtu anapotaka nyumba yake iwe safi, ni dhahiri kabisa lazima aifanye usafi ili iwe safi kama yeye anavyotaka, sasa kwa kufanya hivi si kwamba anaokomoa uchafu la! Bali anaweka nyumba yake kuwa safi kwa sababu mtu yeyote hawezi kuishi nyumba ilyoichanganyikana na uchafu.
Vivyo hivyo na kwa Mungu wetu Mungu awachomi watu katika ziwa la moto kwa sababu ana wakomoa kisa katuumba yeye lakini kama ilivyo kwa mwanadamu jinsi apendi kuishia na takataka, ambazo zikizi sana huzichoma, vivyo na kwa Mungu wetu YEYE NI MTAKATIFU kama ni Mtakatifu ni wazi kuwa hawezi kuchangamana na maovu na lengo kuu la Mungu kuwachoma watu, ni ili kuondoa maovu maana yeye hakai katika ya uovu, ndiyo maana hata shetani baada ya kuasi huko mbinguni Mungu alimtupa dunia na yote kwa sababu shetani alikuwa amejawa na uasi na uovu
Vivyo hivyo nasi tunapaswa tutambue kuwa Mungu anatuvumilia sana na maovu yetu tunayoyafanya, ili tubutu tuepukane na Hilo ziwa la moto, usiseme moyoni mwako kuwa nitatubu siku nyingine, unachelewa ndugu maana saa ya wokovu ni sasa, tubu Leo na umwamini Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, ili uwe salama
Ufunuo wa Yohana 2:11
[11]Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Ikiwa utapenda kuongozwa sala.ya toba unaweza Kufungua link hi>>
Au ukawasiliana nasi kwa namba hapo chini
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.