KOIKOI ANGANI AJUA NYAKATI ZAKE ZILIZOAMRIWA.Una maana gani huu msatari katika yeremia 8:7

Maswali ya Biblia No Comments

Koikoi ni ndege wa kubwa
Wenye miguu mirefu na mdomo mrefu na mwembamba Ndege hawa wana rangi nyeupe, kijivu na nyeusi. Sasa turudi kwenye maandiko tuone yanasemje juu ya hawa ndege na ni upi ufunuo na hekima tunaweza kuipata hapa kama watoto wa Mungu na ikatusaidia katika maisha Yetu ya wokovu.

Yeremia 8:7 “Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana”.

Hawa Koikoi na mbayuwayu na korongo ni ndege wa tofauti sana na ndege wengine, ni ndege wanao tambua majira na nyakati katika ulimwengu huu na kujua ni hatua gani wachukue kipindi fulani kinapokaribia, Na hiyo imewasaidia sana kuishi maisha yasiyo weza kuwaadhiri wao, pasipo kukumbana na kadhia zozote  zile ambazo zisizo za msingi.

Ndege hawa ambao ukifikia msimu wa baridi wanahama wote waeneo yao wanayoishi kwa muda, na kwenda umbali mrefu sana, kwenye upande wa pili wa dunia kuufuata msimu tulivu aidha wa vuli au  wa joto ulipo wakatulie, kisha baadaye hali ya baridi ikishakwisha wanarudi katika makazi yao ya awali kuendelea na maisha yao.

Sasa baridi tunayoizungumzia ni ile baridi Kali sana, ya kuwepo barafu iliyopo huko nchi za ulaya, na baadhi ya nchi nyingine mfano kanada ambazo hata mtu wa kawaida akikaa nje muda mchache tu anageuka kuwa jiwe la barafu, haijalishi atavaa masweta au makoti makubwa kiasi gani.. Baridi ya namna hiyo watu wanaoishi huko wanatumia muda wao mwingi kuwepo ndani, na hata kazi zao wanazifanyia ndani katika nyumba zilizojengwa kitaalamu kuhifadhi joto ndani, kwani nyumba za kawaida kama hizi zetu, kule hazijengwi kwasababu zinapitisha baridi, kiasi kwamba ukikaa ndani yake huko mpaka asubuhi ukiamka umeganda. Huku kwetu Afrika hatuna baridi ya namna hiyo.

Sasa, ndege hawa, wanafahamu vizuri kwa namna yeyoyote Ile hawawezi kuishi katika mazingira hayo ya baridi kali, kwasababu hata viota vyao vitaganda.. Sasa ili kujilinda na tatizo hili inawabidi wahame kwa muda flani ndio hapo waondoka kwenda maelfu ya kilometa wanakuja mpaka huku kwetu Afrika, au sehemu zingine zenye joto, wanakaa  huko mpaka msimu wa baridi  utakaposhakwisha kule Ulaya ndio wanarudi sasa, kuendeleza maisha yao ya kawaida.

Sasa Mungu ametumia hawa ndege kama mfano kwetu ili kutushangaa sisi wanadamu wenye akili timamu kwanini hatujui hukumu zake alizoziweka hapa duniani..anasema..

Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana

Hii ina tumaanisha kwamba tunashindwa kujua wakati wa neema ni upi, na wakati wa hukumu za Mungu ni upi.. Sisi tupo tu hatujui waKati au majira yetu, tunadhani wakati wote, hii neema ya wokovu itaendelea kuwepo, tunadhani wakati wote, hali itakuwa kama ilivyo sasa hivi, tuna fikiri kuwa injili tuta isikia siku zote kama sasa

Wapendwa tufahamu kuwa neema hii inakwenda kuisha siku sio nyingi, Dhiki kuu kubwa ambayo haijawahi kutokea tangu dunia iumbwe na wala haitakaa iwepo itakwenda kutokea ulimwenguni kote..Dalili zote zinaonyesha, pengine katika wakati wetu huu tunaoishi tutayashuhudia hayo..Haya majira ya neema ndio yanaendea mwisho hivyo, muda huu tulionao ni wa nyongeza tu, dunia ilibidi iwe tayari imeshakwisha tangu zamani, lakini kwasababu tu ile nuru ndogo ya jioni ipo ndio maana unaona mambo bado yapo hivi

Sawa tume shafikia wakati ambao Bwana wetu Yesu hatuhubirii  tena injili ya kutuvuta kwenye wokovu, kama ilivyokuwa zamani bali anatuhubiria injili ya kuthibitisha ulichokiamini. Ona anavyo sema

Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo”.

Tunaona sasa yote ni kwasababu ya undumila kuwili tulionao sasa, kwasababu kama tunaweza kuyatambua majira ya nchi, kwamba huu ni msimu wa masika na hivyo tunaanza kuyaandaa mashamba yetu kabla ya mvua kunyesha, au tunahama mabondeni mapema mafuriko yasitukute, inakuwaje basi, tunashindwa kuzitambua siku hizi kuwa ni siku za mwisho? Korona inakufundisha nini? Vimbunga haya matetemeko,mafuriko na vilevile hivi vita vinakufundisha nini, Hili wimbi la manabii wa uongo unaloliona leo hii limezuka duniani kwa ghafla linakufundisha nini? . Bado tu hujali, hizo ni dalili za wazi kabisa ambazo zinatutambulisha kuwa tukio la unyakuo lipo karibu?

Yeye bwana alisema..

Luka 12:54 “Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.

55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.

56 Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya”?

Itakuwa ni ajabu Sana tukizidiwa maarifa na ufahamu na hawa ndege tujiangalie sana, tuamke katika usingizi huu mzito tulio lala, hukumu ya Mungu juu ya ulimwengu wote imekalibia sana. Kama bado uja okoka ni afadhali uokoke sasa haraka, mkimbilie Kristo kwa kumaanisha kabisa kwa moyo wako wote akuokoe, kwasababu muda ume isha wa kuendelea kuwepo hapa ulimwenguni.

mbingu na nchi zitapita lakini maneno ya Bwana Yesu hayatapita milele.

MARANATHA.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *