Kuwa kumbe kipya ni nini?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mpendwa karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana Mungu wetu.tunaweza kusoma maandiko kutoka.

Mhubiri 7:29 “Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi”.

Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba katika ukamilifu wote kama kwa Adam na Hawa aliwaumba katika ukamilifu wa Furaha, Amani, Upendo na kumcha Mungu.

Lakini ulifika wakati hawakuridhika na vile alivyowaumba Mungu wakataka kufanana naye na hii ikapelekea kuishi namna yao na kutaka uhuru wao binafsi ikawapelekea wao kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambapo Mungu aliwakataza wasile na nia Yao ilikuwa ni kupata walichokuwa wanakihitaji lakini hawakukipata na hata katika Dunia ya Sasa watu bado wanabuni namna ya kuishi kwa akili zao tu lakini tunaona ndiyo chanzo Cha matatizo kuongezeka.

Hata sasa mambo hayo yanaongezeka tunaona watu wanabadilisha maimbile Yao kwakuwa hayawavutii wengine wanapaka make-up na wengine wanachubua ngozi zao, kuweka kucha za bandia,kuvaa mawigi,pia wengine wanabadilisha maumbile Yao kwa kufanyiwa upasuaji na kutumia dawa Kali.

Hawataki kubaki na asili Ile ya Mungu bali wanataka kuishi kama Dunia inavyoenda na ni jambo lisilompendeza Mungu kabisa.

Hivyo tunatakiwa kuitunza miili tuliyopewa na Mungu huku tukijiepusha na namna za sasa na tumpendeze Mungu katika kila hatua za maisha yetu na tuwe Wacha Mungu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *