Kwanini hekima ya Maskini haisikilizwi.

Maswali ya Biblia No Comments

Swali: Neno la Mungu katika mhubiri 9:16 linasema hekima ya maskini haisikilizwi.

JE na sisi tunapaswa kupuuzia mashauri au hekima za watu maskini? Kama si hivyo, basi Hilo andiko Lina maana Gani?

Jibu: tusome tena..

Mhubiri 9:16 “Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.”

Tunaposoma andiko hilo kwa mstari huo pekee ni rahisi sana kupata maana potofu maana tunakuwa tunasoma biblia bila kufuata mtiririko au kanuni. Sasa kwa majibu yetu sahihi tuanzie mstari wa tatu

Mhubiri 9:13-16

13 “Pia nimeona hekima chini ya jua, nayo ni kama hivi, tena kwangu mimi ilionekana kuwa ni neno kubwa.

14 Palikuwa na mji mdogo, na watu ndani yake walikuwa wachache; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.

15 BASI, KULIONEKANA HUMO MTU MASKINI MWENYE HEKIMA, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.

16 NDIPO NILIPOSEMA, BORA HEKIMA KULIKO NGUVU; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.”

Maskini huyu pamoja na kuwa hakuwa na elimu wala ujuzi mwingi aidha kisiasa n.k lakini anatoa wazo la busara ambalo linakomboa mji usiingie katika vita. Lakini baada ya mji kuokoka na kubaki na Amani yake maskini yule hakukumbukwa Wala kupewa thawabu.

Hivyo tukio hilo linamshangaza sana Sulemani na kusema ” KWANINI HEKIMA ZA MASKINI HAZISIKILIZWI.. angali wana hekima za kiasi hata cha kuukomboa mji dhidi ya vita!

Hivyo baada ya hapo Sulemani anatoa ushauri kwa kusema tuwatafute Maskini na tusikilize mashauri yao, maana baadhi wamepewaa vitu vikubwa

Ndiposa, anasema ni heri kuwa na Hekima kama Maskini huyu

Kuliko kuwa na Nguvu (kifedha, kimwili au kielimu) na kukosa hekima.

Mhubiri 9:16

16 “Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; WALAKINI HEKIMA YA MASKINI HUDHARAULIWA, WALA MANENO YAKE HAYASIKILIZWI.”

Kumbe mpaka hapo tunalo jawabu, kwamba biblia haituasi kutosikiliza mashauri ya walio Maskini, badala yake ” tunatakiwa tusiwe na dharau dhidi yao, badala yake tuwaheshimu maana wapo wenye hekima”

Hivyo basi mpendwa usimdharau yeyote kwa kuona hana uwezo, elimu, fedha kama wewe, badala yake mheshimu Kila mtu maana huyo Maskini huenda amebeba jambo kubwa Tena huenda likusaidie wewe au wanaokuzunguka.

Basi tunaaswa kuchuja Mambo yote maana si kila Maskini ana Hekima, wengine pia ni wajinga. Pia kwa upande wa pili hata si Kila tajiri anazo akili au hekima, la! wengi hawana hekima pamoja na kusifika sana mbele za watu!

Biblia inasema heri kijana maskini. mwenye hekima KULIKO mfalme mzee halafu mpumbavu, tusome.. ( Mhubiri 4:13)

Basi tunapaswa kuwa wanyenyekevu daima, na pia wenye kusikiliza.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *