Misunobari ni aina gani ya miti?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, karibu tujifunze Maneno ya Uzima.

Isaya 55:13 “Badala ya michongoma utamea MSUNOBARI, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.”

Misunobari ni miti Jamii ile ile na Mierezi. Na tofauti kati ya miti hii miwili ni kwamba misunobari huwa haiwi mirefu kama Mierezi, na pia matawi yake huwa membamba zaidi, Lakini kwa sehemu kubwa miti hii inafanana kimatumizi. Ndio maana katika biblia utagundua Kila sehemu inapotajwa Mierezi basi na misunobari itatajwa pia.

Tusome..

Zekaria 11:2 “Piga yowe, MSUNOBARI, maana MWEREZI umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.”

Pia unaweza soma zaidi 2 Wafalme 19:23, Isaya 14:8, Isaya 37:24, Ezekiel 27:5

Miti hii ya misunobari na Mierezi ilitumika sana hapo nyuma katika Ujenzi wa Nyumba za thamani. Misunobari na Mierezi ilipatikana Katika nchi maarufu ya Lebanoni

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *