Elewa maana ya Mithali 27:22 ” Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni”

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Mithali 27:22 “Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.”

Kwanza kabisa tujue maana ya kinu na mtwangio;  hivi ni vyombo vinavyotumika kuponda au kusaga nafaka laini kuwa unga mfano mahindi na ngano. Au wakati mwingine mimea migumu kuwa laini mfano kisamvu hupondwa-pondwa kwanza kabla ya kupikwa.

Mungu anatumia Mithali hiyo kumzungumzia mtu mpumbavu, kwamba hata ukimtwanga kwa ngano kinuni au njia nyingine yoyote upumbavu wake hautamtoka!

Sasa JE? Mpumbavu ni nani?

Angalia, kibiblia neno mpumbavu ni pana kidogo; SI tu kwamba ni mtu mjinga au kadhalika. Tuone mifano michache

  1.  Mtu anayesema hakuna Mungu (mithali 9:13)
  2. Mgomvi (mithali 9:13)
  3. Mtenda Maovu(Mithali 10:23)
  4. Mtu anayeona njia yake ni sawa machoni pake (Mithali 12:15)
  5. Mwenye kiburi (Mithali 14:13)
  6. Mwenye dharau (Mithali 15:5)

Sasa basi, kumbe Mpumbavu ni mtu asiye na Mungu ndani yake

Kwasababu dhambi ndio chanzo cha upumbavu wote ndani ya mtu. Sasa mtu huyu hakuna kinachoweza kutoa upumbavu huu ndani yake, si elimu Sababu ni wangapi wamesoma hata Wana degree zao lakini bado ni mashoga, wazinzi, walevi, watukanaji.

Hata ukimtwanga vipi hautautoa upumbavu wake.

Kumfunga mwizi gerezani, hakumfanyi kuacha wivi, tumesikia mara ngapi mwizi katoka jela kaiba Tena, teja katoka hospitali na karudia Tena dawa za kulevya, kiongozi ameadabishwa dhidi ya Rushwa na baada ya kitambo anakutwa Tena na hatia ya ufisadi. Yaani hakuna nidhamu au Sheria inayoweza badilisha ujinga itabadilishwa maumbile tu na itaendelea.

JE! Ni kipi kitamgeuza?

Ni Yesu Kristo pekee, Ndiye aliyepakwa mafuta kwa ajili ya Ukombozi na ufunguzi wa Watu wa Mungu. Atakaye dhamiria moyoni mwake kumfuata atawekwa huru kweli kweli.

Bwana Yesu alisema..

Yohana 1:12 ” Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”

Ni ahadi ya Bwana kwa kila atakayemwamini, kumsamehe dhambi zake zote Maana alizifia msalabani, hivyo atahesabiwa HAKI Bure kwa neema yake. Pia Atampa uwezo wa kuwa kama Yeye kupitia Roho mtakatifu atakayeachiliwa ndani yako baada ya kuamini.

Hakikisha unafanya Toba ya kweli, na ubatizo sahihi wa maji mengi kwa jina la Yesu Kristo na kutii neno lake.

Na Upumbavu Wote Utaondoka!

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *