Kwanini kuhani Eli alikufa kwa kuvunjika shingo”?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom.

Kifo cha kuhani wa Mungu Eli kilikuwa kwa kuvunjika shingo SI namna nyingine yoyote pia kama funzo kwetu kuhusu UTII dhidi ya Maagizo ya Mungu..

Mithali 29:1 “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa”.

Eli alikuwa kuhani kwa miaka 40, akiongoza pamoja na wanawe wawili [Hofni na Finehasi], lakini wanawe hawa walikuwa ni Waovu sana, waliwakosesha Waisrael kwa tabia zao zisizoakisi Ukuhani na habari zao zilifahamika Kila mahali. Baadhi ya tabia hizo zilikuwa ni kama kutoza dhabihu isivyostahili, uasherati n.k

Kama ilivyo kwa baadhi ya wakristo wa Leo makanisani.

Kutokana na dhambi zao watoto wa Eli ilibidi Mungu awaadhibu, lakini adhabu ikamfikia mpaka Eli kutokana na tabia yake ya kutomsikiliza Mungu na kugeukia zaidi watoto wake (Uovu), kwa sababu aliyajua Maovu ya wanawe akapuuzia.

Eli anaonywa mara tatu, mara ya kwanza anaonywa na Waisraeli, mara ya pili anaonywa na Mungu kupitia Nabii (2samweli 2:29) lakini bado hakusikia, na ya tatu anaonywa na mtoto Samweli kwa kuoneshwa mpaka hukumu ambayo itapatikana kwa wanawe lakini bado aliwaacha..

1Samweli 3:13 “Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia”.

Siku Ile ilipofika Israeli walivamiwa na wafilisti, wakapigwa na wafilisti wakalitwaa na Sanduku la Bwana, tuangalie habari nzima..

1Samweli 4:13 “Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.

14 Naye Eli aliposikia kelele za kile kilio, akasema, Maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli.

15 Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona.

16 Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu?

17 Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.

18 Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini”.

Hivyo kifo cha kuhani Eli ilikuwa ni funzo au kuonesha madhara ya kutotii Maagizo ya Mungu.

Kama Eli alivyokuwa kuhani wa Mungu, hakutii sauti ya Mungu na kufa kwa kuvunjika shingo yake! Je? Si sawa na wakristo wa Leo ambao wanafanya maasi angali wanajiita waliookolewa? Kwa maonyo mbalimbali katika mahubri na mafundisho wameyakataa Maagizo ya Mungu, kwa kusudi? Hii ni hatari zaidi!

Tuepuke vifo vya kuvunjika shingo zetu ghafla kiroho, kwa Kushindwa kurudi tena katika Ile neema ya kweli, kwa sababu ya dhambi ya kusikia na kupuuuzia..

Mithali 29:1 “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa”.

Tuache kushupaza shingo zetu kwa kusudi na tusikie Maagizo ya Mungu, tuache dhambi ambayo haina faida yoyote leo na hata Milele baada ya kifo. Tuzitambue alama za nyakati tunazoishi na tuwe macho. Tubu dhambi zako badilisha mwenendo wako, ukabatizwe ujazwe Roho Mtakatifu uwe mwana wa Mungu upate Uzima wa milele.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *