Karibu tujifunze Maneno ya Uzima.
Nini maana ya kuwatema Farasi? Na kwanini Mungu aliwaagiza Israel kuwatema Farasi wa adui zao?
Tusome..
Yoshua 11:6 “Bwana akamwambia Yoshua, Usiche wewe kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa hali wameuawa wote mbele ya Israeli; UTAWATEMA FARASI ZAO, na magari yao utayapiga moto.
7 Basi Yoshua akaenda, na watu wote wa vita pamoja naye, ili kupigana nao hapo penye maji ya Meromu ghafula; wakawaangukia.
8 Bwana akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza hata kufikilia Sidoni ulio mkuu, na hata kufikilia Misrefoth-maimu, tena hata kufikilia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawapiga hata wasiwasaze hata mtu mmoja aliyesalia.
9 Yoshua akawafanyia vile vile kama Bwana alivyomwamuru; AKAWATEMA FARASI ZAO, na magari yao akayapiga moto”.
Wana wa Israeli chini ya uongozi wa Yoshua walipovuka mto Yordani walikutana za adui zao wengi na wenye nguvu za kivita huko kanani. Mmoja wapo alikuwa Mfalme Yabini wa Azori, aliyekusanya majeshi kutoka mataifa kando kando yake kuwapiga Israeli Alikuwa na Jeshi kubwa lenye magari, farasi za kivita nyingi sana wakifananishwa Wingi wao kama Mchanga wa Bahari.
Lakini Mungu anamuagiza Yoshua kuwa Baada ya kuwapiga adui zao wasichukue chochote na wawateme farasi zao.
Kuwatema Farasi maana yake Nini?
Kutema kuharibu tishu za misuli ya miguu inayowezesha kiumbe kujongea (kupanda, kuruka au kuukimbia). Kwa Binadamu zinapatikana nyuma ya mguu kuanzia gotini Hadi kwenye mapaja, vivo hivyo na kwa wanyama. Mtu au mnyama anapoharibiwa misuli hiyo huwa haiponyeki au kufanyika upya tena Kutembea.
Ni Desturi ya kivita kuwa farasi wasiohitajika hutemwa misuli yao ya miguu ili wasitumike Tena hata na Adui, hivyo wanabaki pasi na matumizi yoyote baada ya hapo.
Sasa ukitazama kwa makini utajiuliza kwanini Mungu asiache Israeli wachukue farasi wale na silaha baada ya kuwapiga Maadui? Na badala yake Mungu anawaamuru kuwatema Farasi hao na kutochukua kitu chochote?
Angalia, ni kwa sababu Mungu alihitaji tegemeo lao Israeli liwe kwake pekee na siyo kwa silaha za kivita Wala farasi, Bali waujue ukuu wa Mungu wao asiyetegemea Nguvu za wanadamu, Aokoaye kwa Roho wake.
Zaburi 20:7 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu”.
Wana Israeli hawakutumia magari Wala farasi za kivita walipovuka Yordani lakini waliogopwa na Adui zao wote, sababu ilikuwa ni Tumaini lao lilikuwa kwa Mungu pekee kuwaokoa.
Hivyo hata sisi leo hatupaswi kuweka tumaini letu mahali pengine popote [Mali au mwanadamu]zaidi ya kwa Mungu wetu
Huku tukiwa tayari tumevaa silaha zote za Imani [Waefeso 6:11-17]. Tumtumaini Mungu wetu naye Atafanya.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.