Maana ya kuota nyoka.

Ndoto No Comments

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu Tuyatafakari pamoja Maandiko

Suala la utafsiri wa ndoto limekuwa suala mtambuka sana. Na kwa bahati mbaya wengi wanakosa tafsiri za ndoto zao, hasa kulingana na Maandiko.
Ni vyema kabla hujatafuta tafsiri ya ndoto yako uyajue makundi haya matatu ya ndoto Ambayo ni Ndoto zinazotokana na Mungu, zinazotokana na Shetani, mwisho ni zinazotokana na mtu mwenyewe ( yaani Shughuli, mazingira yanayomzunguka, mawazo n.k) na hizi Huchukua sehemu kubwa zaidi (95%) na ndoto hizi hazibebi ujumbe wowote! Ni za kupuuzwa.

Tukirudi katika ndoto hii ya kuota nyoka, wengi wamekuwa wakiuliza maana ya ndoto hii. Sasa Cha kuzingatia ni kwamba nyoka kibiblia anasimama kama ishara mbaya.
Endapo umeota ndoto ya namna hii zaidi ya mara moja basi SI suala kupuuzwa, izingatie sana.

Nyoka anaonekana katika tabia kuu tatu yaani kudanganya kama alivomdanganya Hawa pale edeni(Mwanzo 3:1-5), tabia ya kuuma au kugonga kisigino kama ilivyoandikwa ( Mwanzo 3:15), tabia ya kumeza kama alivojaribu kummeza yule mtoto (ufunuo 12:4). Hizi zote ni kazi za shetani, ndiposa anafananishwa na nyoka na SI kiumbe kingine chochote.

Ndoto hizi mara nyingi hutoka kwa Shetani, japo kuna nyakati hubeba ujumbe wa kiMungu.
Inaweza ikaja kwa namna nyingi mfano kuumwa na nyoka, kuviringishwa, kukimbizwa n.k wapo wengine huota wapo baharini au ziwani na joka kubwa linatoka huko lakini yote inabeba ujumbe mmoja nao ni ADUI YUPO MBELE YAKO

>Ibilisi yupo mbele yako aidha kukudanganya; na ikiwa upo nje ya kristo basi tayali unaishi chini Ya udanganyifu wake. Sasa kabla udanganyifu huo haujawa mkubwa zaidi na kuzaa mauti, fungua macho yako na urudi kwa Muumba wako angali mda upo.

>Ibilisi anakutega udondoke dhambini, huenda ikawa ni dhambi itakayogharimu sana maisha yako, jichunguze njia zako chukua tahadhari kwa kufunga milango yote ya mwovu ikutengayo na Yesu Kristo, Maana hapo ndipo mtego wa shetani ulipo.
Ibilisi anakutegea mtego utakaoleta madhara katika Utumishi au huduma yako, familia, afya n.k amedhamiria kukufanya usisonge mbele (kukugonga kisigino)
Kama Mwokozi wetu Yesu alivyotuagiza tuombe sana, ili tusije ingia majaribuni. MAOMBI ni silaha yetu.

Shetani anataka kukimeza kile Mungu ameweka ndani yako
Shambulizi la kwanza ni katika NENO LA MUNGU maana anajua ukiwa na neno utaleta madhara makubwa katika ufalme wake wa Giza; hivyo anafanya Juhudi kukimeza ulichokisikia
Hiyo inafananishwa na zile mbegu zidondokazo njiani ndege wakaja na kuzila
Rejea..

Mathayo 13:18-19

18 “Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.

19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”

Ikiwa Umeokoka fanya Juhudi sana kuulinda wokovu wako kwa Maombi na utakatifu; Maana shetani yupo karibu yako akishindana kwa Kila Hali, lakini kama hujaokoka basi Leo fanya hima uingie ndani ya Kristo kuliko na usalama.

Amua vyema na Mungu atakubariki sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *