Maana ya niliazimu nisijue neno lolote kwenu (1 wakorintho 2:2)

Maswali ya Biblia No Comments

Libarikiwe Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Wakorintho 2:2 “Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.”

Haya yalikuwa ni maneno ya waraka wa mtume Paulo kwa kanisa la Korintho.

Kwa lugha rahisi zaidi tuyaweke hivi.. “Nilipokuja kwenu ninyi Wakorintho Nalikusudia kufahamu yale mnayoyajua kuhusu YESU KRISTO ambaye amesulibiwa! si lingine lolote.”

Ikimaanisha kwamba Paulo Alitaka kuelewa ambacho Wakorintho wanaelewa kumhusu YESU Kristo aliyesulubiwa tu, na si mambo mengine.

JE? Ni kwanini Alitaka kujua Ufahamu wao kuhusu Yesu?

Kwa maana Alijua endapo watamfahamu Yesu kama inavyopaswa, basi na imani yao itakuwa katika Misingi thabiti, lakini wakimfahamu Yesu kwa Ushawishi tu au mapokeo basi Imani yao ni juu ya hekima za Wanadamu

1 Wakorintho 2:1-2

1 “Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.

2 Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.”

 

Pia endapo watamfahamu Yesu wa ishara na Miujiza; Basi na imani yao itakuwa huko kwenye ishara Na Miujiza kama wale Wasamaria(Yohana 6:26) si katika imani dhahiri ya YESU ALIYESULUBIWA.

Sikiliza, Wakimjua Yesu kama Mwokozi aliyekufa kwa dhambi zao, basi Imani yao itakuwa thabiti na ya uhakika, ni Ile itakayopelekea kutubu dhambi zao na kufanya mapenzi ya Mungu ambalo ndilo jambo la muhimu (mathayo 7:21-23).

Hivyobasi hata kwetu sisi kitu Cha muhimu ni kushikilia Ile Imani ya Misingi ( Ambayo inatupelekea kujitakasa na kujiepusha na uovu/ dhambi/ uchafu.

Amina

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *