Majumbe walikuwa ni watu gani (mwanzo 36:15)

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Wetu Yesu Kristo na Asifiwe.

tusome..

Mwanzo 36:15 “Hawa ndio MAJUMBE wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; JUMBE Temani, JUMBE Omari, JUMBE Sefo, JUMBE Kenazi,

16 JUMBE Kora, JUMBE Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio MAJUMBE, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada”.

JUMBE au MAJUMBE walikuwa ni wakuu wa koo, kwa lugha rahisi Machifu.

Majumbe walijulikana na waliheshimika sana katika nchi.

Kazi zao zilikuwa ni kutatua migogoro ya kifamilia, na mgawanyo wa ardhi katika ngazi ya Familia.

Sehemu zingine katika biblia zilizotaja habari za Majumbe ni 1 Nyakati 1:51-54, Ester 1:3, 9:3

Kulingana na Maandiko, Majumbe walioheshimika na kuogopeka sana, katika sehemu zao mpaka nje ya mipaka Walikuwa ni Majumbe wa Wana wa Esau.

Soma..

Kutoka 15:14 “Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika.

15 Ndipo MAJUMBE WA EDOMU wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka”.

Lakini kwa Utukufu na uweza wa Mungu katika Sehemu zile za Majumbe wa Esau waliojulikana sana, hakutoka MKUU WA UZIMA (YESU KRISTO) badala yake anatokea katika Ukoo mdogo sana wa Majumbe wa Yuda! 

Mathayo 2:5 “Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,

6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, HU MDOGO KAMWE KATIKA MAJUMBE WA YUDA; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli”.

JE Umemwamini Yesu na kumpa Maisha yako?.

Kama bado basi hamna haja ya kuchelewa zaidi maana tunaishi

katika Majira ya kurudi kwake;

Njia ya kuelekea uzimani inazidi kuwa Nyembaba na Ile ya upotevuni inafanywa pana kupoteza wengi zaidi, kwa kadri wakati unavyozidi kwenda!

Hivyo mpendwa, usikawie kusimama katika njia ya Wokovu ya Mwokozi wetu Aliyekufa kwa ajili yetu Yesu Kristo.Muda umebaki mchache sana.

Maranatha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *