Mazao yanayotumika kutengeneza pombe ni sahihi kuyalima ?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom.

Jibu: hakuna zao lililoumbwa na Mungu kwa lengo baya mfano kutengeneza Pombe, sigara n.k lakini tatizo linaanza pale linapotumiwa vibaya na sisi wenyewe.

Baadhi ya mifano ni kama vile mtama ambao ni zao la chakula lakini watu hulitumia kuundia pombe, miwa ni sukari lakini watu wengine huundia pombe, kadhalika na kwa minazi, mtama, ulezi ndizi n.k

Isaya 5:20″ Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; WATIAO UCHUNGU BADALA YA UTAMU, NA UTAMU BADALA YA UCHUNGU!.”

Tunaweza kujifunza kwa andiko hili kuwa ni ole kwa wanaotumia vitu vilivyoumbwa na Mungu kwa matumizi yake halisi kufanya vitu tofauti. Mfano matumizi kama vile Ilivyoumbwa kuwa ni Mwanamke na mwanamume lakini watu wanageuza kuwa mwanamume kwa mwanamume, ni sawa na kutia Giza katika Nuru na ole! Ilikwisha tolewa.

Amina.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *