Mkisto anaruhusiwa kutumia miti shamba au kwenda hospitalini?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze!..

Hapana shaka Wala changamoto yoyote ya kiimani kwa Aliye mgonjwa kumtafuta daktari au matibabu fulani. Tatizo ni kuwa watu wengine huhisi kwa kutokwenda hospitali au kutafuta njia nyingine yoyote ya matibabu kama vile mitishamba(aloe vera, mwarobaini n.k) ni kuonesha ukubwa wa Imani yao, na imepelekea kupata matatizo makubwa ya kiafya! Imani yako ipo ndani yako Haina haja ya kujaribu au kujithibitisha kuonesha watu.

Katazo linakuja inapoanza kuhusisha masuala ya kiimani au ibada Fulani ambazo ni tofauti na Ukristo. Mfano masharti kama kuamka usiku kunuwia, hirizi, kuvunja Nazi na vinavyofanana na hivyo.

Maana kwa utaratibu tunajifunza hata katika nyaraka mbalimbali za mitume..

Wakolosai 3: 17 “Na kila mfanyalo, KWA NENO au KWA TENDO, fanyeni yote KATIKA JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.

Mungu wetu pia huponya kwa namna mbalimbali kama Maombi, au hata kwa kutumia madaktari na dawa, hivyo ni vyema kuamini katika Uponyaji wa Mungu, lakini tuwe na Hekima tufanyapo maamuzi ya ni njia gani ya kutumia kulingana na hali halisi.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *