NENO JEHANAMU LINAMAANA GANI?

  Uncategorized

Jehanamu au Jehanum, ni neno lenye asili ya Kigiriki , limetafsiriwa kutoka kwa lugha ya Kiyahudi, Ge-hinnom, linalomaanisha bonde la mwana wa Hinomu.

Eneo hili lipo kusini mwa Yerusalemu lilitumiwa na watu ambao walikuwa hawamchi Bwana,.walitumia eneo hilo kwa kuwatoa watoto wao dhabihu kwa kuwapitisha kwenye moto kwa miungu waliyoipata Kanaani.

Jambo hili lilikuwa chukizo kubwa kwa Mungu na ndiyo sababu iliyowafanya wapelekwe utumwani Babeli.

Tunasoma hayo katika..
Jeremia 7:30 “Maana wana wa Yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu, asema Bwana; wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo, iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi.

31 Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.”

Bwana anawaambia wana wa Yuda kwamba wamefanya maovu machoni pake na kuinajisi nyumba inayoitwa kwa jina lake. Wakajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao katika moto. Bwana aliwaagiza wazee wa watu na makuhani kuhubiri maneno ya kwamba Bwana ataleta mabaya juu ya mahali hapa, na masikio ya wale wanaosikia yatawaka.

Yeremia 19:1 “Bwana akasema hivi, Enenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;

2 ukatoke uende
mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia,

3 ukisema, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka.

4 Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;

5 nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu;

6 basi, angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo.”

Mfalme Yosia baadaye alinajisi eneo hilo, na kulifanya lisitumike tena kwa mambo yao ya kichawi. Alitia unajisi Tofethi, ili mtu yeyote asimpitishe mwana au binti yake katika moto kwa Moleki. Eneo hilo lilibaki kutumika kama dampo la jiji, watu waliokufa, takataka na uchafu kutoka kwa jiji.

2Wafalme 23:10 “Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.”

Jambo linatukumbusha pia nasi ndiyo maana
Yesu alitumia mfano huu kueleza picha halisi ya kuzimu kwa wale ambao watakufa katika dhambi zao. Akasema, Mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda jehanamu, katika moto usiozimika, ambamo wadudu wao hawafi, na moto hauzimiki.

Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;

44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]

45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum;

46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;

48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.”

Ni wazi kwamba hakuna mtu anayependa kuwa katika sehemu yoyote chafu, kwa hiyo inatupa motisha ya kuepuka kuzimu. Ikiwa uko nje ya Kristo, wakati ni sasa, tubu, mpe Bwana maisha yako, naye atakupokea.

Je Umempokea Yesu katika maisha yako?. Kumbuka hakuna njia yoyote utakayoweza kumfikia Mungu, au hata kumjua Mungu isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo. Jiulize, ulimwengu umekuahidia nini tangu umeanza kuutumikia? Ukweli ni kwamba haujakupa ahadi yoyote, ya kuendelea kuishi, Lakini Kristo anakuahidia uzima wa milele baada ya kufa, kwanini usichague uzima, na mengine mengi?

Bwana akubariki.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa namba hizi
+225693036618/ +225789001312

LEAVE A COMMENT