Ni alama gani aliyotiwa kaini na Mungu ?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom.

Kaini anapewa hukumu baada ya kumwua Nduguye habili

Mwanzo 4: 9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.”

Kaini anamlilia Mungu akimwambia adhabu aliyompa ni Kali sana, hata Kila atakayeniona ataniua, Lakini Mungu anamuhakikishia Ulinzi kwa kumwambia atamweka Alama..

13 “Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.

14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga”

Swali linakuja ni Alama ipi? 

Tunapaswa tujue kwanza kaini mwenyewe Alijua ubaya wa alama hiyo kuwa ni kutengwa mbali na USO wa Mungu, Na alipo Mungu ndipo penye usalama; Ni kama vile Mwili usiokuwa na kinga utavoshambuliwa na kila ugonjwa, naye kaini alitambua maisha bila fadhili za Mungu kwake jinsi yatavyokuwa, ndipo sasa anatoa kauli hii ya ‘kila atakayeniona ataniua’. Na Mungu anamuhakikishia kuwa atamwekea Alama ili Yeyote asimuue.

Alama hiyo sio ya kawaida labda ya mwilini kama tattoo, hapana! maana isingefanya watu wasimwue. Lakini ilikuwa ni  ukubwa, na  kufikiri ndiyo alama  ya sehemu ya Mwonekano au Ufanisi au sifa fulani tofauti na wengine yaweza kuwa na ukweli zaidi.

Na ukweli kwasababu tunaona uzao wa kaini walikuwa wenye sifa kubwa, Walikuwa wavumbuzi na wenye elimu kubwa (Mwanzo 4:21-22), hodari na wengine wenye Maumbo makubwa (Mwanzo 6:4). Hata Leo tunaona wenye maendeleo ya kielimu na kiteknolojia jinsi ilivyo Ngumu kupigwa kivita.

Lakini uzao wa sethi nduguye, hawakuwa na ujuzi mwingi zaidi ya kilimo na ufugaji lakini ulikuwa ni Uzao wa Mungu.

Kizazi Cha kaini kilitawala Dunia, hawakuwa dhaifu na yeyote aliyejaribu kuwaua, kisasi kingemrudia mara saba kwa jinsi walivyokuwa na Nguvu ingawa hawakuwa na Mungu.

TUNAJIFUNZA NINI KATIKA HILO:

Kumekuwa maswali mengi kwa Waamini kwamba kwanini Waovu wanafanikiwa, wenye dhambi ndio wenye nguvu kivita kiteknolojia na kimafanikio. Unapaswa utambue hiyo ndio Alama yao tangu enzi za Baba yao Kaini. Wangelikuwa Waovu halafu wanyonge wangeishi? Jibu ni hapana!

Kumbe tunajifunza si jambo la kushangaza Mungu kumwakikishia mtu muovu Usalama!

Sikiliza, Usitamani Alama hiyo, ya kulindwa katika Uovu. Maana utalindwa kwa kitambo kifupi baadaye Utaangamizwa katika gharika. Tunajifunza kwa mfano wa ngano na magugu, Watenda kazi walitaka kuondoa magugu ili zibaki ngano, Lakini mwenye shamba akasema waviache vikue pamoja mpaka mavuno, ndipo wayatupe magugu motoni.

Ambapo Ngano ni ulimwengu, mavuno wana wa ufalme na magugu wana wa ibilisi, na wavunaji ni malaika. Kumaanisha duniani hapa zipo pando za aina mbili na zote zitashiriki huduma zote kama mbolea, maji kutoka kwa Mungu, na magugu hustawi haraka kuliko Ngano

Sasa uliye katika dhambi na unastawi kimaisha unastarehe jiulize upo kundi gani? Tambua hiyo ni alama iliyowekwa kwa muda tu, utajiri wako na mafanikio yako zaidi ya Watu wa Mungu ukadhani ndio kibali kutoka kwa Mungu, usipoelewa hilo hapa Duniani Leo, utalithibitisha Hukumuni.

Kubali Leo kuwa mwana wa ufalme kwa kutubu dhambi zako na kumfanya Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako, ili akuondolee deni la dhambi na uwe Mtakatifu kwa damu yake nae atakuepusha na Hukumu ya Mungu inayokuja

ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *