Ni chemchem ipi inatoka ndani yako, ya mito au kisima?

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU..

Ikiwa mtu amelikiri jina la Yesu na kuamua kumfuata Kristo, ndani yake hutoka chemichemi ya maji yaliyo hai (Mithali 4:23)na Yesu ndiye hutoa maji hayo ambayo hayakauki…


Maji hufanya kazi zifuatazo
1.Kuondoa kiu
2.Kumeesha
3.Kuondoa uchafu
4.Kugharikisha ikiwa yatazidi

Hata katika moyo wa mtu maji hufanya kazi hizohizo, yanaondoa kiu ya kufanya mambo mauovu (Ufunuo 21:6, Yohana 4:14), hufanya mambo ya Mungu kumea ndani ya moyo wa mtu, huondoa uchafu ndani ya moyo wa mtu na higharikisha kazi zote za adui.


Maandiko yanatuambia pepo akikemewa na kutoka ndani ya mtu huenda njia ambayo haina maji, ni kwa nini afanye hivyo? Hii ni kwa sababu yale maji yaliyo moyoni mwa mtu humgharikisha pepo na hivyo hawezi kukaa sehemu kama hiyo

Luka 11:24 Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,

25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka

26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza

Kila mtu anayemwamini Kristo hupewa neema ya kupata maji haya lakini maji haya huwa yametulia kama ya ‘KISIMA’ basi ili maji haya yatiririke na kwenda mbali kama maji ya ‘MITO’ inampasa mtu wa Mungu afanye kitu cha ziada.


Maji ya mito hitiririka na kwenda mbali na kuwa faida kwao japo hawajui yalipoanzia, kwa mfano wakazi wa Kilimanjaro hutumia maji yanayotiririka kutoka mlima Kilimanjaro lakini wengi hajui yalianzia wapi japo wananufaika nayo. Tunaona katika maandiko Mungu alitoa mto katika bustani ya Edeni na ulienda nje ya bustani na kuwanufaisha mataifa mengine (Mwanzo 2:10-14)

Basi ikiwa mtu ameokoka na kupata neema ya maji ya kisima basi anatakiwa kufanya jambo la ziada ili maji yake yatiririke kutoka nje.
Kuna wakati mitume walishindwa kutoa pepo sugu na wakajiulza kwa nini,

Yesu aliwaambi hivi

Mathayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]


Ni nini hiyo haitoki? Ni chemichemi ya maji uliyonayo ndani yako, ili upate mabadiliko chemichemi yako itiririke inabidi uwe mtu wa kuomba sana tena kuomba bila kukoma.

Mtu anayeomba huuvuta uwepo wa Mungu katika maisha yake. Maombi ni ‘pump’ inayovuta chemichemi iliyo ndani ya mtu itiririshe maji nje ili na wengine wafaidike na maji hayo. Hakuna namna utawasaidia wengine kama huombi, huwezi kupata maono au mafunuo kama huombi…

Unatamani mumeo aache tabia fulani lakini huombi, unaweza kupona wewe lakini hutaweza kusaidia wengine wapone. Unatamani familia yako imjue Mungu na huingii gharama ya kufunga na kuomba basi ujue yatabaki kuwa matamanio tu labda Mungu awaguse tu yeye mwenyewe.

Lakini chemichemi hii si kwa ajili ya wengine tu bali hata katika yale mambo makubwa ambayo unatamani Mungu aingilie kati unahitaji kuyatoa maji hayo yaende katika mambo hayo. Biblia inatuambia imetupasa kumuomba Mungu siku zote bioa kukata tamaa (Luka 18:1)hii ndiyo njia pekee itakayotupa majibu..

Yohana 7:38  Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *