Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na libarikiwe sana.
Swali: Tunasoma unabii juu ya masihi (katika Isaya 53:12) kwamba atagawiwa sehemu pamoja na Wakuu.. Sasa JE Wakuu hao ni akina nani? Na ni sehemu gani watagawiwa pamoja?
Jibu: tusome..
Isaya 53:12 “Kwa hiyo nitamgawia sehemu PAMOJA NA WAKUU, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini ALICHUKUA DHAMBI ZA WATU WENGI, Na kuwaombea wakosaji.”
Mstari huu unazungumzia ukweli kuhusu masihi (Bwana Yesu)
Na unatafsiriwa hivi “Kuna Wakuu wanaoishi, ambao Bwana Yesu atapewa sehemu pamoja nao”
Mtazamo huo si sahihi kimaandiko; maana JE? Ni mwanadamu Gani awezaye kulinganishwa na Yesu Kristo? Hakika Hakuna!
Sasa tafsiri sahihi ya mstari huu ni hii..
” Mungu atamgawia sehemu Bwana Yesu Kisha atawagawia sehemu na WAKUU”
Na sehemu hiyo ni mji wa Kimbinguni yaani YERUSALEM MPYA
Kama ilivyoandikwa katika (ufunuo 22:9)
Na Wakuu wanaozungumziwa ni WATAKATIFU (Walioishi maisha ya unyenyekevu duniani kama watoto wadogo) Mathayo 18:2,3 soma pia Luka 7:28
Mathayo 18:2-3
2″ Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”
Hivyo sehemu ya Bwana Yesu ni kiti Cha enzi Cha MILELE, Na sehemu ya watakatifu walioshinda au WAKUU ni YERUSALEMU MPYA.
Wanadamu watakaokosa katika kundi la Wakuu biblia inasema hatma yao ni katika ziwa liwakalo moto wa kiberiti
Ufunuo wa Yohana 21:8 ” Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI.”
Wapendwa, tupige mbio kwa Juhudi kubwa ili tukapate sehemu moja pamoja na Bwana Wetu.
Na tuwe wanyenyekevu kama watoto wadogo, tuchukie Dunia na mambo yake, tutafute haki ya Mungu na tusimame imara.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.