Ni sawa kuingia kwenye shamba la mtu mwingine na kula upendavyo?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom.

Turejee..
Kumbukumbu 23:24 Uingiapo katika shamba la mizabibu la jirani yako, utaweza kula zabibu za kukushibisha, kama upendavyo; ila usitie katika chombo chako.

25 Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako.

Maagizo haya yalikuwa katika kipindi Cha Sheria ya Musa (torati), kwa Israel, pia ni vizuri kuelewa kuwa alikuwa akizungumzia ukiwa na Hali mbaya kabisa ya njaa na huna namna nyingine ya kujiponya usife na njaa ndipo ufanye hivyo.

Haikuwa kwa namna yoyote Bali katika Hali Ambayo utakuwa na njaa sana na huna namna ya kujiponya na hiyo. Lakini wafanyapo hivyo hawakuruhusiwa kufunga katika vikapu au mifuko yao, wale Kisha waondoke.

Kwa kipindi hicho kwa Wayahudi Walipewa hiyo kama Sheria. Lakini hatuwezi kuitumia Leo sisi Mataifa, maana kwanza sio utamaduni wetu, huwezi ingia katika Shamba la mtu ukafanya hivyo na kusema, “imeandikwa”, utakuwa umekosea maana ujumbe ule SI kwa nyakati zetu, Wala haikulengwa kuwa Sheria kwetu (mataifa).
Tuwe makini tusomapo Maandiko Matakatifu (Agano la kale) maana lilikuwa likiongea kwa vivuli na mifano sio ujumbe husika moja kwa moja..

Waebrania 10:1 “Basi TORATI, kwa kuwa ni KIVULI cha mema yatakayokuwa, wala SI SURA YENYEWE YA MAMBO HAYO…..”

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *