Nakusalimu kwa Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tena katika kujifunza Neno lake litupalo nuru..
Maana halisi ya neno hilo “kuiaua nchi” ni kuitembelea nchi au kuizuru, mfano mzuri ni kwa watalii pale wanapokuja kwa ajili ya kutalii kutoka katika nchi zao, au wale watu wanaotumwa kwenda kupepeleza nchi fulani, huko ndiko “kuiaua nchi”
Kwa maana nyingine ni kuipeleleza nchi. Yaani kujua jinsi ilivyo na vitu gani vilivyomo na wenyeji wa humo wanakaaje..
Tusome
Waamuzi 18:2 “Basi wana wa Dani wakatuma watu wa jamaa zao, watu watano katika hesabu yao yote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, KUIAUA; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hata nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko”
Je kiroho jambo hili lipoje?
2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake…”
Ukisoma pia
Mithali 15:3
[3]Macho ya BWANA yako kila mahali;Yakimchunguza mbaya na mwema.
Umeona hapo hata kwa Mungu wetu, yeye pia huaiua dunia, akiwatazama wanadamu, aliowaumba je wanashika aliyoyaagiza, na zaidi huangalia watu wanaofanya mapenzi yake na kuwabariki..
Lakini si Mungu tu anafanya hivi hata adui yetu shetani naye pia huwa anaiaua dunia akizungukazunguka ili kuwaanguaha watakatifu wa Mungu
1 Petro 5:8
[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Hivyo tudumu katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu hata atakapo kuwa akituzama basi atufaurahie sisi wanawe, vivyo hivyo tuwe makini kwa huyu mshitaki wetu ili asije akatuangusha TUDUMU KATIKA KUYAISHI MAAGIZO YA MUNGU..
Jina la Bwana litukuzwe..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.