Nini maana ya mstari huu (matendo 21:25) Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kipi?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe Karibu tuyatafari maneno ya uzima

Chakula kinachozungumziwa hapa ambacho kimetolewa sadaka kwa sanamu ni chakula ambacho kimepewa au kimetolewa maagizo ya kishetani ili kitumike mfano katika mambo ya kimila au kwa waganga na wachawi.

Ndiyo hapo utakuta kabila Fulani wanafanya tabiko, kisha wanatumia mnyama yeyote labda mbuzi, ng’ombe, labda kwa ajili ya kuweka ulinzi fulani, alafu baada ya hapo wanakula kile chakula, hichi kitendo ni ndiyo kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu..

Au watu waoenda kwa waganga kisha wanapewa maelekezo au masharti, waleta mnyama ili watengeneza dawa kwa ajili ya tatizo alilolipeleka, kisha baada hapo anaambiwa ashiriki kile chakula ili kusababishe utatuzi wa tatizo, huyu mtu naye anakuwa ameshiriki vyakula vya maagano ya kipepo

Ndiyo maana mtume Paulo alilisema hili

Matendo 21:25 “Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati”

Kwa mtu ambaye tayari umempokea Kristo Yesu maishani mwako hupaswi kabisa kujihusisha na mambo hayo na mfano ikitokea labda umekula pasipo kujua kama chakula hicho kina maagano haina shida lakini kama umefahamu na bado unaendelea kula unakuwa umefanya kosa, kwa sababu kama mtu akifanya hivyo inasabisha hatari katika Roho yake

1 Wakorintho 10:19-22 “Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?

20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.

21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

Ikiwa umeshawahi kushiriki mavyakula haya ya kishetani, maagano ya kimzimu bila kujua, basi jua kabisa ndani yako una ushirika na mashetani, lakini Bado lipo tumaini la kutoka huko endapo utampokea Yesu Kristo maishani mwako, naye atatakasa maisha yako utakuwa salama na utatoka katika hayo maagano nawe utawa salama …

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *